The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo anazungumza muda huu lengo ni Uhamasishaji wa Kutoa Elimu a Nishati Safi kwa Viongozi wa Baraza la Wazee Arusha
Karibu kufuatilia kinachoendelea.
View: https://www.youtube.com/live/jEzBkft9o9g?si=uw038dewWr2M8B72
Akizungumzia ushirikishwaji wa kundi la wazee katika Kutoa Elimu ya Nishati Safi
"Tunayo kampeni inayoendelea ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya masuala ya nishati safi ya kupikia, kampeni ambayo inakwendaa kuokoa mazingira yetu, na ambayo sisi kwenye mji wa utalii tunatakiwa tuipigie chapuo zaidi kwa sababu utalii na mazingira vinaendana. Makundi mengi yameshirikishwa, walemavu, akinamama, vijana na makundi mengine yote, tulikuwa tumebakiza kundi hili la wazee."
"Wazee wote hawa kila mmoja nyumbani kwake ana jiko la gesi, lakini tukasema ni vizuri baada ya kampeni hii unapokwenda mwalimu kufundisha ni lazima upewe kitendea kazi na kwenye masuala ya nishati safi kitendea kazi ni jiko la gesi la kupikia, kwahiyo tumeona leo baada ya kumaliza mazungumzo yetu ya leo tutaweza kutoa jiko la gesi kwa kila mzee ili anapokwenda kule nyumbani akatusaidie kutoa elimu. Kila kata watu saba jumlisha na viongozi kwenye ngazi ya wilaya tukapata idadi yao 182, tutahakikisha watu wote 182 majiko hayo ya gesi yanawafikia mpaka walipo."
Akizungumza kuhusu uteuzi wa Dtk. Samia kuwa mgombea urais kupitia CCM
Amesema Chama cha Mapinduzi na wanachama wake wameshafanya maamuzi ya kumteua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea wa Urais hivyo wanaopiga kelele wanapaswa kukaa kimya kwa sababu wao sio wanachama wa Chama hicho.
"Watu wengine wanadhani kwamba Dkt. Samia ameteuliwa lakini kiuhalisia amechaguliwa kwa sababu sisi kwenye mkutano mkuu tulipiga kura ya kumchagua kuwa mgombea wetu, sasa ukiona mtu mwingine chama sio cha kwake CCM wenyewe tumekaa tumesema sisi 2025 mgombea wetu ni Dkt. Samia Suluhu Hassan, sasa wewe yasiyokuhusu unapiga porojo zako unapoteza muda, kakae kwenye chama chako, katafute mgombea wako tukutane uwanjani uchaguzi mkuu"
Akizungumza kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anapaswa kuongezewa miaka mitano ya uongozi ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kwa ufanisi.
"Kama kuna mtu anadhani kwamba hii kazi ni nyepesi, anapoteza muda. Matendo ya Dkt. Samia yanaishi, yanaonekana, na tunalazimika kumwongezea miaka mitano ili kazi hii iwe ya kudumu. Hatuhitaji mtu wa kuja kujifunza au mtu wa kupiga porojo, tunahitaji mtu ambaye anajua anachopaswa kufanya na tayari ameshaanza kufanya,"
Vilevile ametumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Jimbo la Arusha Mjini, akibainisha kuwa serikali ya Rais Samia imewekeza katika sekta mbalimbali ili kuboresha maisha ya wananchi.
Akizungumzia uborshaji wa miundombinu unapojengwa uwanja wa mpira wa miguu.
"Dkt. Samia ameona ukijengwa uwanja tu, miundombinu kule ni mibaya sana, uwanja bila miundombinu hali itakuwa ni mbaya sana, Mama Samia amebariki na amewatuma wataalamu wake wa TARULA na taasisi nyingine kuhakikisha wanakwenda kwenye lile eneo na wafanye usanifu wa masuala ya barabara ili uwanja ukikamilika waweke na barabara za lami ili iwe rahisi kwenda kwenye lile eneo la uwanja"
Azungumzia kuelekea uchaguzi 2025
"Yapo baadhi ya majimbo, akishapita kiongozi wakati wa kampeni kurudi Majaliwa, sisi hapa Dkt. Samia hakauki,na kwakweli katika majimbo yanatakiwa yashindane kumpa kura ni Jimbo la Arusha na Jimbo la Dodoma mjini kwa sababu haya ndiyo maeneo anayokwenda mara nyingi"