Kama kuna mambo yanachukiza basi ni huu unafiki wa kiwango cha SGR. Moderator naomba msifute.
Hivi karibuni huyu kijana ameonekana "akijaribu" kwa kiwango kikubwa sana kujitenganisha na Utawala katili na dhalimu wa Magufuli, kitu ambacho hakijui ni kwamba hawezi kukwepa sehemu udhalimu huo.
Jana alisikika "akikandia" uporwaji wa Bureaus uliofanywa na serikali ya Magufuli huku yeye akiwa Mkuu wa Mkoa husika na akakaa kimya kwa wakati huo! Jana anadai kuwa kitendo hicho hakikua cha kibidamu.
Leo ameibuka tena baada ya watu wenye akili kuhoji kauli zake hizo, Leo anadai kuwa UTAWALA ule haukumpa nafasi yeye kama RC kutenda haki na majukumu yake yalitekelezwa na "Junior" wake kwa kisingizio cha "maelekezo kutoka juu".
Namkumbusha Gambo kuwa, hata huo Ubunge alionao Leo hapo anajua fika kuwa hakustahili kuwepo hapo, hivyo namshauri AJENGE HOJA aache kutukumbusha machungu ya ndugu zetu waliofilisiwa na Utawala dhalimu wa mwendazake
View attachment 1819779