Mrisho Gambo acha Unafiki

Watu msilielie chamuhimu tubadili katiba ili Rais asigeuke mfalme!! Kwasasa ningumu kumkatalia Rais na ukabaki salama hata supika alisema mkubwa akishasema wao hawawezi kumbishia wanakaa kimya...
hasahasa rais asiependa mawazo mbadala kama mwenda!!
 
Isipokuwa kwa ugonjwa wa akili siko pamoja na wewe...Mengine yote nakubaliana nawe
 
Watu Kama Hawa hata mama Rais Samia awe nao Makini Sana asije akawateua kuwa mawaziri Ni wanafiki Sana watakuja kumgeuka nayeye pia.Tena uyu hata ubunge hajapata kwa Sanduku la kura leo anamshambulia boss wake wa zamani.
 
Ivi mnadhani kwenye utawala wa yule dhalimu Kuna mtu ambae angethubutu kwenda kinyume chake?? Au mmesahau yaliyomkuta Nape Nnauye na wengineo wengi
Angeomba kupumzika nafasi yake sio taaluma Ile watu wapo wengi wanaweza kuwa wakuu wa mkoa kwanini aliendelea kutii maagizo ambayo anaona ni kandamizi? Uyu ni cheo tu anataka apewe uwaziri ndo target yake
 
Uovu wa kupora ubunge wa Lema mbona hauongelei.Aachie ubunge ili tumuone kweli anachokiongea anakimaanisha na hapendi dhuluma.
 
Msimuonee Gambo kujifanya hamtambui Hali halisi..pr ya Gambo chuga Ni njema..huwez kumfananisha na sabaya..

Kazi take ilikuwa kuioiga chadema ili achukuwe ubunge....

Hakuwahi kuwaumiza watu personally...

Binafsi simchukii
 
Inawezekana kwa mtu mwenye imani na roho ya ubinadamu kama yeye roho yake ilikuwa inaumia kwa uovu waliokuwa wanafanyiwa wananchi na hasa wale ambao aliteuliwa kuwaongoza

shida ni kwamba yeye kwa nafasi yake Kama mkuu wa mkoa kwa wakati huo alitumwa kusimamia utekelezaji wa mipango ya Bwana mkubwa bila kujali kwamba yataumiza wanaotakiwa kuutumikia mpango wenyewe ama laa na tusisahau ya kwamba ingemgharimu sana kupoteza kazi ama hata maisha au kuishia magereza kama angepingana na mipango ya bwana mkubwa ambaye ni bosi wake kwa wakati huo

hivyo tuelewe tu ya kwamba watu ama viongozi kama Gambo walikuwa wanaumia sana kwa uovu uliyokuwa ukitendeka na kama alivyosema ama kuandika yeye mwenyewe kwamba bwana mkubwa angeweza hata kumtuma mtu wa chini yako kwenda kufanya mambo ya ajabu bila hata ya kukuripotia wewe ambaye ndiye mkuu wake wa kazi
 
Kama aliumia na akakaa kimya, tutaaminije kuwa hatakuja kuumia na kukaa kimya tena?
 
Tuna vijana vigeu geu na wasiokuwa na misimamo thabiti, vijana wa aina hii sio wa kuamini na wanaweza kuuza nchi kabisa
 

..nakubaliana 100% na ulichokisema.

..lakini KATIBA yetu inawapa nguvu MADHALI kuliko watetezi wa haki.

..kwenye nchi zenye katiba nzuri Mrisho Gambo angeweza kupinga hayo ma-task force na sheria ikamlinda yeye na kumuadhibu aliyeunda ma-task force.

..Kwa mfano, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Georgia alikataa mashinikizo ya kupika matokeo toka kwa Donald Trump. Na aliweza kufanya hivyo kwasababu wenzetu wameandika katiba na sheria zao kwa namna ambayo haitoi mwanya kwa madhalimu kuwaadhibu wapenda haki.
 
Sasa bosi ni nani? Huyu unayemuita bosi waty wanamsubiri kwa hamu huko gereza la segerea 😂
 
Rais Samia amerithi mihimili iliyotengenezwa kuishi KINAFIKI....!

Ni jukumu lake kurejesha ustaarabu na uungwana katika mihimili hiyo.
 
Mkuu kwa kauli hizo amenajisi integrity, uaminifu wake katika mamlaka za kuteua anakosa sifa sasa na hata milele, inahitaji mjadala wa kifalsafa kuhusu ukatili na udhalimu kumuhusu Magufuli. Mungu ampe pumziko jema na lenye heri huko aliko hasa tu kama aliofanya yalikuwa kwa nia njema kwa Tanzania na Watanzania wa sasa na wa baadae, Kwenye socio-economic transformation nayabeba mabaya yake when i see europe, asia, amerika, kinshasa, south africa, it will take presumably 20-50yrs kutakuwa na misafara ya Hija kwenda kaburi la Magu na siku ya kifo chake itaadhimishwa kwa kumbukumbu ya fahari. Sitakuwa na objection na mtamzamo kinzani wa aina yoyote ila maana mawazo mbadala ni afya na tanuri jema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…