Mrisho Gambo ajijue yeye sasa hivi ni Mbunge sio Mkuu wa Mkoa tena

CCM msituchoshe bana ... mnajitekenya wenyewe mnacheka wenyewe ... mnalazimisha hamasa wala watu hawana time na nyinyi ... serekali yenu na watendaji wake haina mvuto sikwambii hao wabunge ndio kabisaaaaa!

Mnatengeneza malumbano ili ionekane kuna amsha-amsha ya kukimbiza maendeleo ndio mnazidi kuharibu kabisaaaaaa mnaonekana kabisa mnacheza sinema za mzee yombayomba

Mlituahidi Tanzania tutaishi kama ulaya na mkasema wapinzani ndio walikua wanachelewesha maendeleo haya sasa tunasubiri msituletee mapichapicha ya kutengeneza hapa hamna amsha-amsha yeyote Hovyooooo ... !!!
 
....mkimaliza kuwasumbua wapinzani mtahamia wenyewe kwa wenyewe .....
 
Uchawi una tabia moja. Mwanzoni huuwa majirani, lkn majirani wakiisha unaanza kuingia kwenye ukoo wa mchawi na hatimaye humuua mchawi mwenye.

Hiyo ndiyo CCM. Awali CCM ilishughulika na wapinzani. Sasa wapinzani hakuna inashughulikia wanaccm wenyewe.
 
Nondo mbona una kichwa kibovu, huyu gambo nani kamchagua kuwa mbunge? Sema aliyeiba kura na kujipachika ubunge.....
 
Mkuu wa mkoa kaacha ukuu wa mkoa kawa mbunge kajisahahau akifikiri bado Ni mkuu wa mkoa anatembea adi na watendaji,

Alizoea kukoromea mkuu wa wilaya mkurugenzi saivi anakoromewa yeye. Na hataki kuubali ukweli.
 
Hajui mbunge hana tofauti na mjumbe wa nyumba kumi kasoro posho na mshahara.
 
Huyo dogo na limbukeni mwenzake Bashite walifikia mahali wakajisahau na kudhani kuwa wao ndiyo wenye nchi. Gumbo anavuna alichopanda. Alizoea kuwanyanyasa akina Lema asijue kutesa kwa zamu. Ashukuru Mungu amesaidiwa kuiba kura na kuwa mbunge. Hakupaswa kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi. Ana bahati. Naomba Magufuli amuamishie Arusha mkuu wa mkoa wa sasa wa Mbeya ili ampe na kumtia adabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…