Pre GE2025 Mrisho Gambo asaidia Bodaboda Arusha kwa kiasi cha Milioni 1.2 kuboresha Usalama na Utalii

Pre GE2025 Mrisho Gambo asaidia Bodaboda Arusha kwa kiasi cha Milioni 1.2 kuboresha Usalama na Utalii

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amewakabidhi Bodaboda wa Jiji la Arusha kiasi cha Shilingi 1,200,000 kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa kuwezesha kusajili Bodaboda za Jiji la Arusha na kuwezesha upatikanaji wa taarifa za uhakika kwa ajili ya usalama na utalii.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kiasi hicho, Gambo amesema kuwa yeye kama mbunge ni muhimu kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba anaowawakilisha, hivyo kukabidhi kiasi hicho ni moja ya njia za kutatua matatizo hayo.

"Mfumo huu ni kitu kizuri sana kwasababu unajua leo inaweza kutokea ajali ya bodaboda, pengine aliyepata ajali hali yake inaweza kuwa mbaya, akawa hawezi kuzungumza, unataka kumtafuta ndugu yake, taarifa unampataje? Lakini ndani ya mfumo, kuna taarifa za bodaboda na taarifa za wadhamini wake au ndugu zake", amesema Gambo.

Pia, Soma:

Gambo atoa Milioni 2 kulipia kodi ya chama cha bodaboda, awanunulia pia TV wafuatilie matukio duniani

Arusha: Gambo asaidia malazi kwa manusura wa ajali ya moto

Nao viongozi wa Bodaboda Jiji la Arusha wakiwakilishwa na Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina wamemshuru sana Gambo kwa kutatua changamoto zao kila wanapomfikishia na kuwaomba viongozi wengine waige mfano wake wa uongozi wenye kuacha alama.

"Mbunge wetu amekuwa akisaidia si tu Bodaboda, tunaona amekuwa akifanya mambo mengi kwenye vikundi mbalimbali, kwahiyo kazi anayoifanya tunaiona", wameeleza.
 
Back
Top Bottom