The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Safari yetu bado ndefu sana. Ukiangalia mazingira na hali za watu wanaomsifia kiongozi kwa kuwajali sana unaishia kusononeka tu. Hivi wale ambao Samia hajawajali hali zao zikoje?Wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo mkoani Arusha wamemshukuru Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhimiza sera na kuweka mazingira wezeshi ya kufanyia biashara nchini.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa Mbunge Gambo amekuwa akiwawakilisha vyema bungeni kwa kueleza na kupambania masilahi yao hivyo kumtakia yeye na Rais Samia heri katika kuwatumikia Watanzania.
View attachment 3297160