No Reform, No Election. Hivi chaguzi za kijinga kama Polisi na usalama wanataka kuwa vyama vya siasa wajisajili tujue moja. Lakini Watanzania watakuwa wa ajabu kwenda kupiga kura kwenye chaguzi ambazo wanajua kura hazihesabiwi. Hizi reform sio za kusaidia chama kimoja ni za kuongeza uwazi na kuhakikisha kura zinahesabiwa sasa tatizo ni nini. Kama tumeona mfumo wa demokrasia haufai kwanini tunapoteza pesa za wananchi za chaguzi kama hawachagui chochote. Ndiyo maana maamuzi ya Chadema ni ya kizalendo. Wananchi wakikubali ujinga wasije kulalamikia maendeleo au kusema baadae tunaibiwa. Nchi ni watu kama watu wenyewe wakiona powa kudanganya na kura fake za polisi na usalama basi tuendelee lakini Chadema wametoa nafasi kwa chaguzi za serikali za mtaa tumeona.