Pre GE2025 Mrisho Gambo: CHADEMA Wakisusa, sisi twala

Pre GE2025 Mrisho Gambo: CHADEMA Wakisusa, sisi twala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amesema kauli ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya "No Reform, No Election" inaonesha dalili za woga, akisisitiza kuwa CCM ina uzoefu wa kushinda hata pale upinzani unapogomea uchaguzi.

Akizungumza Februari 4, 2025, katika maadhimisho ya miaka 48 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha, yaliyofanyika katika kata ya Akeri, wilayani Arumeru, Gambo alisema:

"Wenzetu wa CHADEMA wanasema 'No Reform, No Election'. Hiyo ni dalili ya woga. Tunataka tuwakumbushe kuwa sisi tuna uzoefu, tushapita Kamati Kuu. Wakisusa, sisi twala."

 
Lema kaikimbia Arusha, anaishi ktk corridor za chama
 
No Reform, No Election. Hivi chaguzi za kijinga kama Polisi na usalama wanataka kuwa vyama vya siasa wajisajili tujue moja. Lakini Watanzania watakuwa wa ajabu kwenda kupiga kura kwenye chaguzi ambazo wanajua kura hazihesabiwi. Hizi reform sio za kusaidia chama kimoja ni za kuongeza uwazi na kuhakikisha kura zinahesabiwa sasa tatizo ni nini. Kama tumeona mfumo wa demokrasia haufai kwanini tunapoteza pesa za wananchi za chaguzi kama hawachagui chochote. Ndiyo maana maamuzi ya Chadema ni ya kizalendo. Wananchi wakikubali ujinga wasije kulalamikia maendeleo au kusema baadae tunaibiwa. Nchi ni watu kama watu wenyewe wakiona powa kudanganya na kura fake za polisi na usalama basi tuendelee lakini Chadema wametoa nafasi kwa chaguzi za serikali za mtaa tumeona.
 
Back
Top Bottom