Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Akichangia bajeti ya waziri mkuu, mbunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo ameongelea sekta ya madini ikiwemo mabadiliko yaliyopelekea kuhamisha soko la madini kutoka Arusha kwenda Mirerani na hasara yake kwa Serikali na mji wa Arusha.
Mrisho Gambo: Mwaka 2019 tulianzisha masoko ya madini, Arusha lilikuwepo, Mererani na maeneo mengine. Tanzanite ambayo inapatikana Tanzania hairuhusiwi kwenda kuuzwa kwenye soko la Arusha.
Maamuzi ya kubadilisha kanuni yameipatia Serikali hasara kubwa sana. Baada ya kuhamishia Mirerani, ukiangalia kipindi kile kile cha July 21 hadi Januari, Serikali imepata kodi kiasi cha milioni 339 kutoka bilioni 1.3, tuweza kuwa na caret elfu 15 kutoka elfu 85.
Kwahiyo unaona maamuzi haya yamekwenda kuitia hasara Serikali. Arusha idadi ya dealers ilikuwa 103 leo kuna dealers 48 tu Mirerani.
TAARIFA: Napenda kumpa taarifa kwamba madini ya Tanzanite yapo mkoa wa Manyara na Serikali imeweza kujiongezea kipato tangu soko liliporejeshwa katika mji wa Mirerani.
Gambo: Ushauri wangu ni wabunge watafute hoja za kuchangia, sio tunadandia tu ilimradi tuonekane na wananchi wetu, hapa tunaongea mambo serious kwahiyo sipokei taarifa yake. Mheshimiwa spika pia kuna ajira zimepotea, ajira zaidi ya 413, mabroker zaidi ya 2,500 wamekosa ajira.