Pre GE2025 Mrisho Gambo: Nitaenda kuwajibu nini wananchi wa Arusha. Jiji kama Arusha linakosaje stendi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Ni wazi sasa Mrisho Gambo ameanza kuchachawa na kukumbuka shuka kukiwa kunakucha.

Ameng’aka bungeni dhidi ya serikali kwa kuhoji kuwa ataenda kuwaambia nini wapiga kura wake wa Arusha mjini kwa Jiji kubwa la Arusha kukosa stendi bora na ya kisasa kama mikoa mingine.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Siku zote hizo alikuwa wapi? Anaona uchaguzi unakaribia anaanza kutoa mapovu na kutia huruma.

Hakika Gambo ni kama ameanza kutapatapa na kwa ushauri mzuri, atafute kazi nyingine tu ya kufanya! Bashite kashammaliza

Gambo ndiye chanzo kutofanyika kwa ujenzi wa hiyo stendi alafu ananyoosha kidole kwa nani?.

Wakati wa JPM pesa ilitolewa, eneo lilishapimwa na mpaka mkandarasi alishasafisha eneo, baadaye wakaanzisha mtifuano kwamba kule mbali, kumbe Gambo and Company wanataka stand ijengwe kwenye eneo lao.

Mzee baba akaona hawa hawaitaji stand, pia soma hii; Kituo Chetu Mabasi Arusha hiki hapa
 
Lema si alisema kaifanya Arusha kuwa Dubai?
 
Gambo ndiye chanzo kutofanyika kwa ujenzi wa hiyo stendi alafu ananyoosha kidole kwa nani?.

Wakati wa JPM pesa ilitolewa, eneo lilishapimwa na mpaka mkandarasi alishasafisha eneo, baadaye wakaanzisha mtifuano kwamba kule mbali, kumbe Gambo and Company wanataka stand ijengwe kwenye eneo lao.

Mzee baba akaona hawa hawaitaji stand, pia soma hii; Kituo Chetu Mabasi Arusha hiki hapa
Siyo Arusha tuu. Mbeya kwenyewe ni aibu
 
Standa ya Arusha ni mfupa mgumu, wengi wamejaribu wameshindwa.
Viwanja vimetolewa mara 3 lkn mradi umekwamishwa na vigogo.

Hili lilimshinda hadi Magufuli.
Arusha ina wenyewe.
Mafisadi ya nchi hii yananufaika kwa mkwamo wa stand kuu.

Hata Magufuli alikwama
 
Back
Top Bottom