The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Mashaka Gambo, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, akibainisha kuwa kampeni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Arusha na maeneo mengine nchini.
Akizungumza Ijumaa, Machi 7, 2025, katika Uwanja wa TBA mkoani Arusha yalipo mabanda ya Wizara ya Katiba na Sheria kunakotolewa msaada bure wa sharia, Gambo amesema kampeni hiyo imerahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi kwa kupunguza mlolongo mrefu wa kesi mahakamani.
Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Alieleza kuwa awali, wananchi walilazimika kupitia ngazi mbalimbali za mahakama, jambo lililochukua muda mrefu. Hata hivyo, kupitia kampeni hii, masuala yanatatuliwa kwa haraka zaidi kwa njia ya usuluhishi na maelewano. Gambo ametoa mfano wa raia wa Italia waliokuwa na mgogoro kwa miaka saba ambao ulitatuliwa kupitia kampeni hii, pamoja na kesi za ndoa, mirathi na madai mbalimbali dhidi ya serikali.
Mbunge huyo ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kusimamia vyema kampeni hii, akisisitiza kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhana ya 4R za Rais Samia, inayolenga haki, usuluhishi, amani na maendeleo.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, inalenga kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi, hususan wale wasiojiweza, ili kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote.
Kampeni hii imekuwa ikitekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo Arusha, na imeonesha mafanikio makubwa katika kutatua migogoro ya muda mrefu na kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi.