PreGE2025 Mrisho Kamba: Jokate ni nguvu mpya ya ushindi wa CCM 2025

PreGE2025 Mrisho Kamba: Jokate ni nguvu mpya ya ushindi wa CCM 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
1,062
Reaction score
1,138
*JOKATE NI NGUVU MPYA YA USHINDI WA CCM 2025
*
Kalamu ya: Mrisho H. Kamba – Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wazazi CCM Taifa

Ndugu Jokate Urban Mwegelo,

Salamu nyingi za pongezi na heshima nyingi kwako. Natumaini ujumbe huu unakufikia ukiwa na afya njema na ari ileile ya kuwatumikia Watanzania, hususan vijana wetu.

Kwa dhati kabisa, napenda kukupongeza kwa kazi kubwa, ya mfano na yenye matokeo chanya unayoendelea kuifanya katika kuwaunganisha, kuwahamasisha na kuwawezesha vijana wa Tanzania kote nchini. Tukio lako la hivi karibuni na vijana wa Seneti wa Mkoa wa Dar es Salaam ni ushahidi tosha wa dhamira yako ya kweli na moyo wako wa kizalendo kwa mustakabali wa taifa letu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Safari yako ya uongozi – kutoka Mkuu wa Wilaya wa Kisarawe, Temeke, hadi Korogwe – na sasa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, ni ushuhuda wa uthubutu, uwezo na maono makubwa. Umejijengea heshima si tu ndani ya Chama, bali pia miongoni mwa Watanzania wengi wanaoamini katika kizazi kipya cha viongozi wachapakazi.

Ninaamini kwa dhati kuwa chini ya uongozi wako imara, vijana wa Tanzania watapata fursa nyingi zaidi za kujifunza, kushiriki, na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa letu – kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Uvumilivu wako, uzalendo wako, na maono yako ni chachu muhimu ya ushindi wa CCM mwaka 2025. Endelea kushika bendera ya matumaini kwa vijana na taifa kwa ujumla. Tunakuamini, tunakuunga mkono, na tunakuombea uendelee kuwa mwanga wa mabadiliko chanya kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Pamoja twajenga Tanzania imara – Vijana ni Nguvu, Jokate ni Kiongozi!

20250408_224512.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20250408_224920_Facebook.jpg
    Screenshot_20250408_224920_Facebook.jpg
    317.4 KB · Views: 35
Back
Top Bottom