Soka Ndio Maisha Yangu
Member
- Nov 27, 2024
- 43
- 127
Mimi nafuatilia sana Siasa za Jimbo la Arusha Mjini, Jana nimemsikiliza sana diwani mmoja akimuomba radhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha akijifanya analilia kama mtoto wa kike aliyenyimwa Kodi ya pango na bwana wake akidai kuwa Gambo amekuwa mtu wa mizozo na migogoro na madiwani wenzake.
Eti amemuomba Mkuu wa Mkoa kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa madai kuwa anaongelewa sana mitaani na wananchi.
Eboo, Jimbo la Arusha Mjini kwa namna nilivyofuatilia kuanzia mwaka 2020 hadi Leo, hakuna diwani atakayerudi pale kwenye Halmashauri ya Jiji.Na sababu ziko nyingi sana, Moja Arusha inakabiliwa na changamoto nyingi kwenye kata, hakuna diwani hata mmoja amewahi kuzungukia kata na kufanya mikutano ya hadhara ya wananchi ya kutatua kero zaidi ya kumsubiria DC au RC, unawezaje kurudi kwenye Baraza la madiwani kwa staili hiyo.
Pili, madiwani wamekaa kimchongo sana, walitegemea Gambo awe sehemu ya wapiga dili wenzako jambo ambalo Gambo amelikataa tangu akiwa DC pale Korogwe.Mimi nimekaa Korogwe miaka 20 namjua Gambo, hana mambo ya kupiga dili hata kidogo, Sasa baadhi ya madiwani wanapomuona Gambo akikataa kumaliza msitu wa Halmashauri wanamuona mkorofi, hafai na sio mtu wa maendeleo.
Gambo ametimiza majukumu yake kama mbunge, Kila siku kwenye vikao vya bunge tunaona kwenye kurasa zake akiuliza swali bungeni, mnataka afanye nini.
KAZI ya mbunge ni kuwakilisha wananchi, kupeleka kero za wananchi bungeni ili zitatuliwe, jambo ambalo Gambo amelifanya sana.
Gambo ni binadamu sio mungu, hatuwezi kusema yupo perfect 100% ila Jamaa anajua namna ya kujenga hoja, kuwakilisha wananchi na kufikisha kero zao.
Gambo hapendi upuuzi na wapuuzi wa aina ya yule diwani ambaye hadi anamaliza miaka mitano ya udiwani hana anachojivunia kwa wananchi wake.
Wapo baadhi ya madiwani na viongozi wa mtaa anaoshirikiana nao vizuri TU na mambo yanaenda, ukiona Gambo hashirikiani na diwani fulani ujue diwani huyo ni mjinga mjinga na hajielewi.
Mimi nasema Gambo atahukumiwa na wananchi wa Arusha kwa hoja zake na sio kelele, ujinga na porojo za wanasiasa wenzake ambao wanawapigia kampeni watu wanaotaka.Gambo navomjua, simpigii debe Wala sifahamaniani naye ila atapangilia hoja zake vizuri sana akiwaeleza wananchi miaka yake mitano ya ubunge amefanya nini.Jiji Zima la Arusha siku hiyo patamea nyasi, Tena nitaomba apewe angalau nusu saa nzima aeleze wapiga kura wa CCM kwenye kura za maoni amefanya nini, ataeleza mambo mengi aliyofanya kama mbunge, sijui kama wapiga kura watachomoka.
Kwa hiyo tuache Siasa za majitaka, kura za maoni