Mrisho Mpoto ana kesi ya kujibu

steering

Member
Joined
Nov 28, 2011
Posts
71
Reaction score
12
Jana usiku akiwa ktk kipindi cha mikasi alikanusha madai ya Watz waishio ughaibuni kuwa ameisaliti Tz Na mlima kilimanjaro na lugha maridhawa Kiswahili. alidai kwa kua kiswahli na ml Kilimanjaro vinajulikana ni asili ya Kenya hivyo deal la kutafsiri kitab cha Shakespere (jina sikumbuki) na kuigiza kwa kiswahili mkenya naye akamtafuta mpoto. siku ya kuperfom (kwenye moja ya nchi za ulaya, jina nalo limenitoka ) alikuta ameandaliwa hotuba ikisema asili ya kisw. ni Kenya kilm nayo pia.
so mpoto alitamka hayo maneno kwa kujitetea; itifaki haikumruhusu kukana yaliyoandikwa. ndipo wabongo waliokuwepo wakamshitaki kwa serikali.mbele ya salama akiwa peku alijitapa yeye ni mzalendo halisi. EATV/m
kasi
 
Kama kweli alikiri Mlima Kilimanjaro upo Kenya basi alikosea sana....
 
Kwenye mambo kama hayo hakuna cha kuzingatia itifaki maana ni usaliti kusema mlima Kilimanjaro upo Kenya.
Hata kama walimlipa kiasi gani angeacha kusoma na ingefahamika msimamo wake.Mpoto wewe si mzalendo.
 
Kwa kweli katika hili Mpoto alipoteza uzalendo na alitutoa katika ramani ya dunia. Binafsi namweshimu sana Mpoto ila niliposikia habari zile kwa mara ya kwanza niliumia mno!
Kama kweli alikuwa mzalendo na mzawa angestop pale pale penye uongo wa kusaliti Tz, naamini hata wazungu WANGEMHESHIMU sana kwani hakuna kitu chaweza shinda uzalendo. Dunia nzima ingesimama kwa muda na hata vyombo vikubwa kabisa vya media duniani vingeripoti tukio lile na dunia ingejua sasa kuwa hizo ni hujuma za Kenya na sasa ukweli ungekuwa wazi na watu kibao wangependa kuja Tz kujiknea ukweli. Nimeumia sana na hakika pesa ni mwanaharamu!
 
huyu jamaa alishawekwa mfukon na magamba ,yako wapi yale masongi ya ukwel ya kukemea ufisad kama mjomba, adela nk? Kweli fedha mwanaharamu
 
Yupo sawa tu kusema upo Kenya,mbona mafisadi wa nchi wameiba madini,wanyama wetu na kusafirisha nje ya nchi na still mnawachagua kila siku kuwaongoza,mwacheni nayeye achukue chake,na ingewezekana nchi hi ingeuzwa na kila mtu akagawiwa hela yake na tukaenda kila mtu na nchi yake anayotaka tukaishi kama wageni,mana ndani ya nchi yetu tumekuwa watumwa.
 
Nilimsikiliza jana wakati akijaribu kujitetea kwa hayo yaliyotokea. Lakini kitu kimoja mimi nilichoelewa ni kuwa, yeye alienda kufanya kazi, na katika ile kazi alipewa masharti na akayakubali ili alipwe. Miongoni mwa hayo masharti ni pamoja na hayo yote yaliyotokea. Alikuwa na uhuru wa kuchagua, kuendana na masharti hayo, ili then alipwe awe na pesa chekwa, au kuyakataa masharti hayo na kuikosa tenda hiyo na kujisifu kwa uzalendo wakati huna pesa. Nafikiri alijiuliza kwa nini yeye ajifanye mzalendo saana aishie kuwa masikini wakati wenye madaraka serikalini wanaimba kuwa ni wazalendo saana wakati wao wao wanakamata Twiga na kuwapandisha Ndege
 
Wakuu mimi niliangalia kipindi kile jana, alichoongea Mpoto hasa ni kuwa ile issue ya kwenda kuperform huko aliletewa na wakenya ambao walikuwa wameaandaa itifaki zote pamoja na matangazo ya TV yeye hakujua kama kuna matangazo ya mlima kilimanjaro, na wala hakujua kama kuna wimbo wa taifa utapigwa. alikuja kushituka pale alipoona wimbo wa taifa wa kenya unapigwa akiwa anaingia kuperfom which means wakenya walimzidi ujanja wakamvalisha ukenya bila yeye kujua. Japo angeweza kukanusha pale pale kuwa mimi ni mtanzania lakini hili linahusu personal instinct sana wengine wanaweza kupata solution ya tatizo haraka wakati mwingine ni mpaka atulie kidogo ndio ajue nini cha kufanya.
 
Hela mwana haramu. Unaweza kumtukana mamako kwa ajili ya hela.

nimeamini kama hilo lilitokea basi fedha ni fedheha.ukifika hapo ni kweli kabisa watu wengine mbele ya fedha ni midabwada na wanaweza hasa kutukana wazazi wao.
 

hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha wewe kuikana nchi yako....huo ni usaliti.
 

dah,,,,
haya sasa bodi ya UTALII imtumie mpoto huyohuyo kuutangaza mlimaaaaaa
 
Alimwambia Adela anyooshe kidole hana nia mbaya ya kumrudisha darasani.. Ni darasa lipi na Adela ni nan sasa mpoto ni zamu yake kunyoosha kidole kwan hatuna nia mbaya ya kumrudisha darasani (darasa la wazalendo wenye kujivunia nhi yao popote katika hali yoyote) by the way hana moyo wa kitanganyika na huo ni UFISADI
 
Kwa hili hawezi kukwepa lawama kwa namna alivyoweka tumbo mbele na kusahau kwamba anajizalilisha mwenyewe kwa kukubali kununuliwa na kukubali jambo ambalo anatambua siyo kweli.

Kwa namna yoyote hawezi kusema kwamba hakutambua kuhusu hiyo hotuba kwa kuwa huwezi ukaletewa hotuba mkutanoni na kuisoma ,ni lazima uipitie kwanza ili kujua inazungumzia nini na kujiandaa kwa masuala ambayo yatahitaji ufafanuzi au maelezo ya ziada.

Nilimheshimu sana kwa kuona jinsi anavyoitangaza nchi na utamaduni wake kumbe ni WALE WALE WACHUMIA TUMBO AMBAO WAPO TAYARI KUSALITI WENZAO/TAIFA KWA FEDHA.

Kwa kosa kama hili inatakiwa hatua kali zingechukuliwa lakini km aliyeiba anapewa muda wa kurudisha kile alichobakiza uzalendo utatoka wapi!
 
haya ndo matokeo ya tanzania kutojali na kuthamini wasanii wake. yeye alikua akisaka mkate wa kila siku. Serikali yenyewe imeshindwa kuutangaza mlima mpoto ndi ataweza?. Wabaneni viongozi wa nchi hii wawe wazalendo ndo sisi tufuate. wapi meremeta na deep green?. mia
 
na Tanzanite ni Mpoto ndo kaenda kusema huko soko la dunia kwamba inatoka kenya na south afrika,kuweni makini
 
hehe turipa saa 72 riwe rimeondoka nchini. Chezeya njaa veve. Aisee hata mimi lazima nisaliti mbele ya pesa kwa serikali hii ya chama cha mipasho sorry mapinduzi ijapokuwa sijui walipindua nini oh nimekumbuka walipindua azimio la arusha, walipindua ndugu kuwa mheshimiwa walipindua uzalendo kuwa ufisadi kutokana na mapinduzi hayo hata mimi nitapindua jina la tz kuwa kenya na kuwa fisadi ili nipate chapaa hivyo simlaumu mpoto ila kama angefanyahivi wakati chama cha mapinduzi hakiko madarakani ningemlaumu. Go mpoto kweli Mungu yu mwema nitajivunia nini nchi yangu wakati haijivunii mimi kuwa mwananchi wake? nitajivunia nini nchi yangu wakati wenye pesa wako juu ya sheria? nitajivunia nini nchi yangu wakati muda wowo inaweza kuchukua roho yangu na kufanywa kama kuku wa mfugaji ambaye muda woote aweza amua kuniua?
 
alimueleza mjomba mjomba hakumsikia so bora akawaeleza wajomba wa majirani wanaweza msikiliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…