Elections 2010 Mrithi wa Dr.Slaa Karatu amepatikana...

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Posts
4,132
Reaction score
1,577
Leo katika Jimbo la Karatu mrithi wa kiti cha Ubunge katika Jimbo hilo amechukua fomu kwa maandamano makubwa na kusindikizwa na wananchi wa mji wote wa Karatu.

Huyu anaitwa Israel Yohana Natse. Alikuwa mkuu wa Jimbo KKKT ,Jimbo la Karatu .
 
Mpaka leo alikuwa kazini na hivyo kuchukua kwake fomu kutamfanya ajiuzulu kazi yake, wananchi wa Karatu ndio walimfuata na kumtaka yeye ndio awe mgombea wa kiti hicho.

CCM hawataambulia chochote kwenye jimbo hilo , na hivyo mapambano dhidi ya ufisadi kuendelea.
 
Another good news kwa Chadema every little move counts
 
Jimbo na Halimashauri vitaendelea kuongozwa na CHADEMA , na hivyo wale wote ambao walikuwa na hofu eti Jimbo litapotea waodoe shaka .
Ntawawekea wasifu wa huyu bwana punde .
 
Asante tuwekee huo wasifu, wakati CCM wakiendelea kugombana na rushwa yao Chadema endeleeni kujipanga kwenye majimbo msihofu kuwakaribisha watakaoona wamechezewa rafu ndani ya CCM maana wote ni watanzania wanaopigania taifa lao la tanzania.
 
Ha ha ha Nasikia CCM wanataka kuwafanya Wananchi wa Karatu ni Vilaza sana kiasi cha Kuwaletea Mtu anayeitwa Dr. Wilberd Slaa ili eti wananchi wachanganyikiwe He he he Inabidi wananchi wa Karatu waiadhibu CCM kwa kuwadharau Kiasi cha kuwaona wao hawawezi Kutofautisha kati ya Dr. Wilbroad Slaa ( Mtetezi wa Wanyonge) na Dr. Wilberd Slaa
 
Leo katika Jimbo la Karatu mrithi wa kiti cha Ubunge katika Jimbo hilo amechukua fomu kwa maandamano makubwa na kusindikizwa na wananchi wa mji wote wa Karatu.

Huyu anaitwa Israel Yohana Natse. Alikuwa mkuu wa Jimbo KKKT ,Jimbo la Karatu .

Duh....ametoka Padre anaingia Mchungaji!!
 
Mmmh! Nahisi huyu sio mgeni jf amebadili jina tu! Ila tabia, sura mawazo ni yaleyale kazi unayo. Lile jina la mwanzo lilikuwa bovu! Hongera Good stratergy
 
Duh....ametoka Padre anaingia Mchungaji!!
Hata angekuwa Sheikh,wanachohitaji wananchi wa Karatu ni uongozi bora.Mkiishiwa hoja mnakimbilia kwenye udini,na ndio maana kuna umuhimu mkubwa wa kuiondoa CCM sasa kwa vile katika desperation zenu za kung'ang'ania madaraka mko tayari kututumbukiza kwenye religious conflict.
 
Mpaka leo alikuwa kazini na hivyo kuchukua kwake fomu kutamfanya ajiuzulu kazi yake, wananchi wa Karatu ndio walimfuata na kumtaka yeye ndio awe mgombea wa kiti hicho.

CCM hawataambulia chochote kwenye jimbo hilo , na hivyo mapambano dhidi ya ufisadi kuendelea.

waamuzi ni wananchi wa karatu, na mpira siku zote ni dakika tisini
 
Kama ni Mch na Mwl Natse, basi jimbo la Karatu litaendelea kuwa mikononi mwa CHADEMA. Huyu alishakuwa Mch wangu huko Machame-Lyamungo Kati kabla ya kwenda masomoni na kisha kuwa mkuu wa chuo Mwika Bible School. Kabla ya kuitwa kuchunga kondoo wa Bwana alikuwa mwalimu. Ni mtu makini sana sana asiyecheza na uchafu (Mr clean). Hamumunyi maneno linapokuja swala la kusema ukweli. Ana sifa nyingi za kuwa kiongozi.
 
Ha ha ha Nasikia CCM wanataka kuwafanya Wananchi wa Karatu ni Vilaza sana kiasi cha Kuwaletea Mtu anayeitwa Dr. Wilberd Slaa ili eti wananchi wachanganyikiwe He he he Inabidi wananchi wa Karatu waiadhibu CCM kwa kuwadharau Kiasi cha kuwaona wao hawawezi Kutofautisha kati ya Dr. Wilbroad Slaa ( Mtetezi wa Wanyonge) na Dr. Wilberd Slaa
Huyo ndo mtu mwenye akili kuliko wote huko CCM aliyegundua hiyo mbinu!! Sijui picha wataifanyaje!!
 
Tanzania is for chadema. nukta. huyo muisrael wa chadema anaonekana kuwa na mwanzo mzuri
 
Huyo ndo mtu mwenye akili kuliko wote huko CCM aliyegundua hiyo mbinu!! Sijui picha wataifanyaje!!
Makamba ndiye alitoa wazo hilo la kutafuta mtu mwenye jina linalofanana na Slaa hata kama hana uwezo, wakampata Dr. Willibard Slaa hiyo ndiyo akili yao ya mwisho kulipata hilo jimbo, nasikia Makamba aliitwa gineus kwa kutoa wazo hilo.
 
hizo ndo akili za opportunist MAKAMBA.
 
Back
Top Bottom