SI KWELI Mrithi Wa Ufalme Wa Kuwait Adai Kuokoka, Atangaza Imani Kwa Yesu Kristo!

SI KWELI Mrithi Wa Ufalme Wa Kuwait Adai Kuokoka, Atangaza Imani Kwa Yesu Kristo!

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Katika kile kinachoonekana kama tukio la kihistoria na lisilotarajiwa katika ulimwengu wa Kiislamu, taarifa kutoka Mashariki ya Kati zinaeleza kuwa mwana wa kifalme kutoka familia ya kifalme ya Kuwait, anayefahamika kwa jina la Prince Abdullah Al-Sabah, ametangaza hadharani kuwa ameokoka na sasa ni mfuasi wa Yesu Kristo.

Katika faili la sauti lililorushwa kupitia kituo cha televisheni ya Kikristo cha Al-Haqiqa, kinachorusha matangazo kwa lugha ya Kiarabu, sauti inayodaiwa kuwa ya Prince Abdullah inasikika akitangaza kwa ujasiri kuwa amemkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.


Katika ujumbe huo wa sauti, Prince Abdullah anasema kwa uthabiti kwamba:

“Iwapo nitauliwa kwa sababu ya rekodi hii ninayozungumzia wokovu wangu, naamini kwa moyo wangu wote kuwa nitakutana uso kwa uso na Yesu Kristo.”

Hata hivyo, hatua hiyo imezua mtafaruku mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Kiislamu, ambapo baadhi ya Waislamu wamejitokeza wakikana kuwa yeye ni sehemu ya familia ya kifalme ya Al-Sabah – familia maarufu ya kifalme inayoitawala Kuwait, taifa tajiri kwa mafuta.

Jina Abdullah (ambalo maana yake ni mtumishi wa Mungu) ni jina linalopatikana mara nyingi kwenye ukoo wa kifalme wa Al-Sabah, jambo linaloibua maswali mengi juu ya uhalisia wa madai hayo.
Kuwaiti-Royal-Prince-Converts-to-Christianity.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwa na chapisho ambalo limechapishwa na mtandao instgram kupitia account ya gospeltothe nationastz wakieleza kuwa kuwa Mrithi Wa Ufalme Wa Kuwait Adai Kuokoka, Atangaza Imani Kwa Yesu Kristo!

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli.

Ufuatiliaji kutumia maneno muhimu JamiiCheck imebaini kuwa taarifa hiyo imekuepo mtandaoni kwa kipindi kirefu angalau tangu mwaka 2012 na wala si ya hivi karibuni. Tazama hapa kuona baadi ya vyanzo vilivyoongelea taarifa hiyo mwaka 2012.

Licha ya taarifa hiyo kuwepo mtandaoni kwa muda mrefu lakini hakuna uthibitisho wowote unaothibitisha jambo hilo. Picha inayoonekana kwenye chapisho hilo ni ya Sheikh Mubarak Abdullah Al-Mubarak Al-Sabah ambaye pia anatokea familia ya kifalme na hakuna mahali panapoonesha kuwa aliwahi kubadili jina.

Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa hakuna ushahidi unaoonesha kuwa jina la Abdullah Al Sabah halina uhusiano wowote na ufalme wa Kuwait wala kuwa mrithi.

Badala yake kuna jina la Ahmad Al-Abdullah Al- Sabah ambaye ni mchumi, mwanasiasa na pia amewahi kuwa waziri wa mafuta kuanzia mwaka 2009 hadi 2011.
Back
Top Bottom