loulla
Senior Member
- Jun 11, 2016
- 125
- 91
Habari. naomba masaada wa kisheria. Baba yangu alimuuzia rafiki yake eneo baada ya kumuomba wakae wote karibu na hali ya kuaminiana. baada ya kuuziana tu, rafiki yake akaanza kuumwa na kufariki akiliacha eneo chini ya uangalizi wa baba maana tangu anunue hakuwai kufika wala kuliona tena, kipindi kichache alichokua akija alikua akija na wanawake tofautitofauti na kua alikua na watoto ila hawakuwai kufika, ni miaka 11 sasa inaenda 12, ametokea mwanamke mmoja kati ya aliowai kuja nao anaonekana alikua hawara mpenda mali, amekuja na documnts nyingi tunazoisi amezipata kwa njia ambayo si halali, kwakua anadai ni msismamizi wa mirathi ila hajawai kufika na watoto wala ndugu wa marehemu. siku ya kwanza kuja alikuja na mteja na baba alimkatalia kwa kudai hamfahamu na anaitaji watoto wafike ili wasije wakazurumiwa, pia hua hafiki kwenye eneo moja kwa moja anaishia kwa wapimaji wa viwanja akiwa na lengo la kupatiwa hati miliki. Naomba msaada wa kujua tufanyeje.