MtoMsimbazi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2009
- 1,800
- 3,091
Kuna rafiki yangu anaishi na mkewe ila jamaa alimkuta mkewe na mtoto moja na yeye akazaa nae mtoto moja hivyo dada anawatoto 2 na rafiki yangu anamtoto 1, tatizo lililopo baba wa mtoto anapiga simu saa 3 usiku anataka kuongea na mwanae na pia mdogo wa mtoto wake kupitia simu ya mke wa rafiki yangu je hapa kisheria huyu mtoto anatakiwa ( au mazingira) ya huyu mtoto wa kwanza (mwenye baba anaepiga simu saa 3 usiku ) yanatakiwa yaweje ili nimsaidie rafiki yangu kwakuwa anakwazika sana na simu za jamaa wakati wa usiku.