Msaada aliyeniuzia ploti anainyemelea

Msaada aliyeniuzia ploti anainyemelea

Piento

Member
Joined
Feb 18, 2018
Posts
5
Reaction score
0
Anadai kwenye hiko kieneo kuna kaburi sijui alizika mtt mchanga kipindi cha nyuma sana, af sasa kile kikaratasi tulichoandikishana nabkutia saini nmekipoteza naishije apo, sheria inasemaje nikipoteza iyo hati ya mauziano pili kuhusu iyo ishu ya kudai kuna kaburi apo nifanyeje???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie ahamishe hilo kaburi kwenye hilo eneo jipya. Kwani kaburi kitu gani bana? Septic tank ni kaburi kubwa tunaloishi nalo. Ng'ombe wote tunaokula, wanaishia huko!
By the way, pesa ulimpa mkononi au kwenye akaunti?
 
Kama una uwezo jenga hapo fasta hata kama ni chumba kimoja ukae maana washenzi kama hao wanaingiza tamaa wakishaona umekaa muda mrefu bila kujenga
 
Kifupi huyo jamaa amekuona fala hupaswi kumchekea, nina uzoefu kidogo na hii migogoro ya ardhi, fuata ushauri wa mdau hapo juu, jenga hata chumba kimoja tena kajenge kwenye hilo eneo analodai kuna kaburi na ukikitana nae usijitie mnyonge wala usimpe kabisa muda wa kujadiliana kuhusu hicho kiwanja akitaka labda umuuzie tena kwa bei unayoitaka wewe, pia jaribu kujenga mahusiano mazuri na majirani wengine simaanishi ujipendekeze, ukiona wanazingua wakazie jenga kisha pangisha au muweke mtu akae hata bure!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saw mkuu, Nashkur sana

Kuna watu hapa duniani wana akili balaa..
 
Pole sana Mkuu kwa hali iliyokukuta. Mimi sio Mwanasheria ila matatizo ya ardhi mengi nishawahi kuyashuhudia na nimejifunza mengi sana na ushauri wa Wajumbe hapo juu uzingatie.Jenga kibanda hata cha chumba kimoja na mtafute ndugu yako yoyote akae hapo hata bure kwa lengo la kukulindia eneo lako ili hata huyo jamaa akija akute kuna mtu anaishi.

Pia ogopa sana kumuweka mtu baki mana kuna tatizo lilitokea Mbezi Beach ambalo mwenye ardhi alimuweka mtu baki ili amuangalizie eneo na pindi mtu baki alivodanganywa na hela za wajanja wa mjini,akapokea almost 5 Mil then akakimbia anakokujua yeye na Mhusika akajenga haraka na siku jamaa anakuja alipata mshtuko wa ghafla so watch out kwa hilo.

Pia hata huyo mtu wako ukimuweka,tafadhali msainishe mkataba wa kukaa na kukuangalizia eneo na pia awe anasimamia usafi wa hilo eneo.

Hayo ni mawazo tu
 
Back
Top Bottom