Msaada: Ana 'D' mbili o'level anataka IT

Msaada: Ana 'D' mbili o'level anataka IT

Sultan Kipingo

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
238
Reaction score
178
Habari wakuu
Nahitaji ushauri wenu juu ya mwanafunzi aliyemaliza form 4 na kupata division 4 ya 32.

Na hizo D mbili alizonazo si ktk masomo ya sayansi yani hesabu, fizikia, kemia, baiolojia ama jiografia.

Binafsi anahitaji kusomea Information Technology IT au kozi zinazoenda na kozi hii ktk vyuo vinavyotambuliwa na serikali yani sio vile vya mitaani.

Alijaribu kurudia mtihani mara mbili lakn hakuweza kupata zaidi ya pointi hizo.

Vyuo vingi vya fani ya compyuta vinahitaji mtu awe angalau na D tatu ili aweze kusomea fani hizo.

Wakuu Ushauri wenu ni muhimu sana juu ya hili.
Ahsanteni.
 
Km sayansi hajafanya vyema there z no way akasoma hiyo it
 
Mkuu mimi nasoma IT level ya degree unajua IT sio kitu rahisi watu wanavyodhani na wala si ngumu ila kwa huyo bora asahau tu akafanye mengine maana huku kuna hesabu na teminology za kufa mtu na kama kingereza pia kina mpiga chenga na ni mvivu wa practical works ataishia kuchekeana na computer tu
 
aende pale dit kuna short courses nyingi aungeunge, ila kwa long course hana sifa, pia hata pale veta chang'ombe wana short course kibao za it.
 
Hiyo ni ngumu mkuu hasa kwa vyuo vilivyo under nacte,ajaribu jomo kenyata arusha labda anaweza pata certificate lakini hakipo chini ya nacte.
 
Hivi mtu aliyefeli form four anaweza kurudia form two bila matatizo yoyote
 
Mpeleke veta mikumi au veta chan'gombe atasoma cheti kwa hatua ya kwanza adi ya tatu kila hatua ni mwaka mmoja akimaliza kwa ufaulu mzuri ataweza kujiajiri mwenyewe au akitaka kuendelea anaweza kujiunga na chuo chochote(Haswa DIT,MIST,Mzumbe)Kwa ngazi ya Ordinary Diploma na baada ya hapo anaweza kuunga degree.Hivyo vyuo nilio kutajia ninauwakika navyo wanapokea wanafunzi wa Veta walio fanya kozi ya mda mrefu na kufaulu vizuri.
 
Back
Top Bottom