Msaada anaejua bei ya miti nataka kuivuna

Nahisi atakuwa amekosea labda alimaanisha 100,000 hadi 130,000 kwenye kuandika ila kama ni kweli basi hiyo ni biashara kichaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee tatizo mnakalili sana mkisikia mtu akiwaambia ukiwa na miti heka moja wewe tajiri(haya mambo nayaona sna humu JF kuwa baadaya miaka 10 eiti unashika milioni kadhaa e.g. 20Milioni ahahahah) mtakuja kufa aisee mkikutana na ukweli kwenye ground, kiukweli miti ni changamoto sana na bei ya elfu 10 na elfu 15 ni ya kiwango cha juu sana ila kawaida miti tunanunua hadi elfu 3 na elfu 7 kutokana na shamba lipo umbali gani na barabara, lipo eneo linalofikika au mabondeni na umbali toka shambani na eneo la soko lambao hivyo vyote vinaamua bei ya miti yako

sasa tukija kwenye uhalisia unaona miti ya miaka 13 inaweza kufikia elfu 15 kama tu ilipandwa kwa nafasi nzuri na ni minene, ipo karibu na barabara hakutaitaji vibarua wa kutoka mbao kutokea bondeni kuja barabarani na gharama za kupeleka mashine ya kupasulia ni ndogo hapo ndio bei yaweza ikawa hiyo. Ingawa kwasasa soko la mbao halijakaa vizuri hivyo changamoto bado ipo kwa wahitaji wa mbao pia miti ipo bei ya chini sana tofauti na miaka mitatu nyuma kipindi ambacho kulikuwa na boom ya bihashara ya mbao.

Lingine la kuongezea kaka ni kwamba sasa bihashara ya mbao imeingiliwa na TRA hivyo mfanyabihashara analipa VAT na hivyo kufanya wengi wa wafanyabihashara wakubwa kuachana na mbao na kufanya mkulima kuteseka zaidi kiasi kwamba sisi dagaa wa mbao tunanunua msitu kwa bei angalau tofauti na zamani kwa mfaa zamani msitu wa 10M sasa ni 3M unapata pia usiashau mpaka upate mbao kutoka kwenye mti kuna gharama nyingi sana za uendeshaji, kuna dalali anayekutafutia shamba, kuna chainswa kukata na kusanzua, Vibarua kukusanya magogo na wale maopereta kwaajili ya kukupa mbao zako hivyo unakuta kwenye mbao moja unakula mia 500 na usipoangalia vizuri kwa kipiga mahesabu kabla ya kununua inakukata

Ndio maana wengi wa wafanyabihashara wa mbao hawapasui wananunua kwa watu mbao sio shamba la miti kwani vijana wengi wamekatika mitaji yao
 
Ulinunua miti iliyopandwa umbali wa mita ngapi mti mpaka mti? Kwa miti ya miaka 13 inaweza simama kwa bei ya 10,000. mpaka 15,000. kama ilipandwa kitaalamu na udongo mzuri.
Kumbe ukiwa na laki tatu tu,unaweza nunua shamba la hela moja...!!
 
kwa upande wangu ningekushauri ukakodi mashine upasue mbao mwenyewe then uje uuze dsm, kuuza miti utaambulia hasara tuu.
Hilo hasijaribu kabisa itamkata mazima, yaani kama alipanga atapata 10M utashangaa mpaka anamaliza kuuza mbao zake ana 4M baadaya ya kutoa gharama zote, kuna kitu kipo kwenye mbao mtu anayepasua mbao unaona misitu yake anauzia wafanyabihashara wengine wakupasua sio yeye anapasua ingawa na yeye anaenda kununua misitu ya kupasua sehemu ingine

Hivyo namshauri huyu jamaa aje auze shamba lake ila asijaribu kupasua kuna changamoto nyingi sana HUU NI USHAURI TU ILA ANAWEZA FANYA VYOVYOTE ATAKAVYO KWAKUWA NI HIYO NI MALI YAKO ILA NIMEMPA ANGALIZO TU
 
Yes boss, ndio mana amekuja hapa kutafuta mawazo so mwisho wa siku yeye ndio atakaa chini aone achukue lipi
 
Kuna mtu kaniambia yuko tayari kunipa mil.5 kwa heka. Nimemwambia ngoja kwanza. Ila mimi heka 4 zote nilinunua mil.3.5

Sent using Jamii Forums mobile app
uza haraka mkuu kwan kwama kila ekari ni m5 inamaanisha 5,000,000÷600= 8300 kila mti kwa sasa ni bei nzuri mno tena sana so 5,000,000×4= 20,000,000 wewe ulinunua zote ekar4 kwa m3.5 ukitoa gharama za utunzaji na muda bado kuna hela nyingi utabaki nazo afu hapo watu watakwambia uwekezaji wa miti ni kichaa fikiria ungekua na ekari hata 30 ungekuwa mbali sana
 
Hebu wapotezeeni wanaosema uwekezaji kwenye miti ni biashara kichaa. They dont know what is long term investment..
 
Hebu wapotezeeni wanaosema uwekezaji kwenye miti ni biashara kichaa. They dont know what is long term investment..
Sana kaka mkubwa kila mwaka panda ekari mbili au zinunue sehemu tofauti tofauti utakuja kunishukuru.
 
Miti inalipa ukiwa na subira
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sahihi kabisa,biashara ya miti inafanyikia shambani,baada ya mtu kuona,kuridhia,hapo lazima aangalie shamba lipoje bondeni au juu,umbali kutoka shamba mpaka barabarani.

Magogo yanaweza kutolewa au mbao kuchaniwa humo humo,miti yako mbao zinazoweza kupatikana kwa wingi ni size gani kwa kipimo 2*2,2*3,2*4.2*6,2*8, 1*3,1*8 vipimo vingine huchanwa kutokana na oda.Mwenye mali nenda tafuta mteja mwende naye shambani au uchane mwenyewe.
 
Ok poa ntazingatia ushauri wako. Lakini sjafika shambani miaka km 4 hivi shida kule mvua zinanyesha sn. Kila nikitaka kwenda nikimuuliza mwenyeji wangu anasema hali ya barabara si nzuri. Juzi juzi hapa alipoenda shamba kuangalia ndo akaniambia miti iko tayari km nataka naweza kuivuna.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda mkuu,huko mvua kunyesha ni kawaida yake,nenda ukaone na uhalisia wa mali yako ipo kama vile ulivyonunua,pita hapo mafinga mjini madalali wapo wengi we jifanye unaulizia biashara ya kununua msitu na kuuza mbao,bei zimekaaje.

Ukitoka hapo unatoka na picha kamili,na ukikuta kipindi misitu ya serikali imefungwa basi malimisitu binafsi bei huwa juu,ile ni mali yako nenda kaithaminishe wewe,muangalizi hachelewi kuingiwa na tamaa au kupata shida akaanza kupunguza mmoja mmoja.nenda shambani.

Fika mafinga pale ongea na wadau kama unaulizia ulizia tu mambo na hali ya soko utavijua,biashara ya misitu haifanywi kwa remote control nenda pale mkuu,siku tatu tu utakuwa ushaamua.
 
Kuna kijiji kinaitwa Kilosa kwa mbele kidogo ila kunafikika sema sina uhakika kwa mvua za msimu huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Panafikika tu,mabasi yapo,piki piki zipo,labda changamoto iwe njia ya kutoa mali shambani,na siku hizi kuna viwanda vya wachina wanamenya magogo kutengeneza marineboard/plywood nenda uliza wananunua shilingi kwa mita za ujazo(cubic meter)
 
Chana mwenyewe.
Njoo mjini utafute wateja uuze.
Au kama vipi kodi sehemu kwa muda weka mtu uza..
Mbao Ina hela ikifika mjini.
Hakikisha ukishavuna unazipiga dawaa mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poa ntazingatia ushauri wako.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…