Msaada: Anakojoa damu na usaha, ugonjwa gani huu?

Henry 14

Senior Member
Joined
Aug 13, 2016
Posts
118
Reaction score
37
Habarini wanajamvini

Nina rafiki yangu wa kiume 24 anasumbuliwa na
-maumivu makali wakati wa kukojoa

-kukojoa damu
-kukojoa kama usahaa

Na inafika wakati anakojoa mpaka anaanguka.

Tumejaribu kwenda hosp tumeambiwa uti , amechoma sindano wapi , kunjwa dawa wapi

Please naombeni msaada tufanyaje, maana hali inazid kuwa mbaya kila cku
 
Kuna ugonjwa zamani tulikuwa tunauita GONO hivi hadi siku hizi upo au?
 
Kacheki Magonjwa ya zinaa...Gonjwa hili limezua kizaazaa gumzo kwa mabronzo ,walimu na wanafunzi by Uswahilini matola(kosa la marehemu)
 
Ugonjwa wa zinaa wahii hospital ukichelewa una stage unafika hauwez pona
 
Mara yake ya mwisho kufanya zinaa lini? kama juzi au jana basi inawezekana ikawa GONOREA au kama aliogelea kwenye maji ya mto inawezekana ikawa kichocho. Mpeleke hospitali afanyiwe vipimo sio kuangaliwa na kupigwa shindano tu.
 
What is UTI ???.Huu ni ugojwa ambao Watanzania asili mia 95 (95%) hawaujui vizuri.Hata baadhi ya matabibu wamekuwa wanachanganya wagonjwa kwa kiwango kikubwa katika kutoa elimu ya afya kuhusu UTI.LAKINI pia alieongoza kwa kwa kiwango kikubwa kuwapotosha Watanzania kuhusu UTI ni nini, ni daktari bandia Dr.Mwaka aliefungiwa kutoa huduma ya tiba mbadala.Huyu kamwaga sana Sumu ya uongo kwa sababu alikuwa anafundisha kupitia redioni na kwenye tv.Kwa faida ya wale wataopata nafasi ya kusoma mada hii basi watakuwa wameilewa UTI ni nini.UTI ni maambizo yeyote kwenye njia ya mkojo.Na maambikizi kwenye njia ya mkojo kwa kiwango kikubwa husababishwa na magonjwa ya ZINAA.Magonjwa ya zinaa ni kama;Kisonono(neisserie gonorrhroe),Clamydia trachomatis,Trichomonas,fungus(candidiasis),herpes simplex virus type 2.Dalili kuu za magonjwa haya ni maumivu wakati wa kukojoa,kuwashwa wakati wa kukojwa,mkojo kuwa wa njano,wakati mwingine kukojoa damu au usaha.UTI kwa kiwango kidogo inaweza kuletwa na magonjwa ambayo sio ya ZINAA kama kichocho cha kibofu cha mkojo(Schistosoma haematobium),vimelea vya Escherichia coli(E.coli),vimelea vya Staphylococcoci na Streptococcoci)Kwa hiyo msaada kwa huyu mwenzetu ni kwamba inaonesha dhahiri ana maambukizo kwenye njia ya mkojo(UTI)Na hayo maambukizo yaweza kuwa kwa kiwango kikubwa ni magonjwa ya zinaa ambayo kwayo hata wewe ni mhanga.Kama wewe hujisikii kitu na tayari mmefanya tendo la ndoa basi wewe utakuwa 'carrier'unaeeneza kwa wengine bila ya wewe kuumwa.Au mwenzako atakuwa amechepuka.Namna sahihi ya kugundua tatizo la UTI ni kupima mkojo,utoko wa njia ya mkojo kama usaha kwa kufanya wet preparation,gram stain na culture.Matibu ya UTI yanategemea na aina ya vimelea vitakavyogundulika kwenye vipimo.Ref.kuhusu UTI unaweza kusoma kwa undani kitabu cha Merck Manual of Medical information.
 
Samahani nilikuwa na maana 'kamwaga sana sumu ya uongo'
 
Mkuu tyupa namna Madasa nimekuwa nikipimwa na kukutwa na uti takriban mwezi wa nane hiv xaxa....na nimetumia dawa za kila aina bila ya kuwa na nafuu na nimekuwa nikipata mkojo wenye chembe chembe kama ya usaha hasa mkojo wa kwanza na hemophilia dawa hali hiyo hupungua na mwingine kibofu kuwasha kwenda sehemu yAw juu ya tumbo na joint za miguu kuuma

Naomba ushauri wako na culture nimefanya kama tatu bila ya kuota kitu chochote
 
Process ya kufanya culture kidogo hua ndefu na wapimaji wengi huvunja maadili ya kazi kwa kulipua kwa kugonga mhuri wa culture kuwa hakuna kilichoota.Wengine hua hawana kabisa vipimio kama culture media na mashine ya incubator lakini pesa ya mteja wanaitaka kwa hiyo hapo lazima ubambikizwe tu.Tatizo lingine yaweza kuwa unatibiwa peke yako na wakati huo huo unaendelea kufanya mapenzi na mwenzi wako ambae anavimelea vya ugonjwa.Halafu jinsia yako ni nani.Kama uko Dar na kweli unaumwa tuwasiliane binafsi nitakusadia kikamilifu hata bila kukupima chochote na utapona 100%.
 
Joint za miguu kuuma hiyo sio UTI bali una matatizo mengine na daktari mzuri anaweza pia kujua unasumbuliwa na vitu gani vingine.
 


Hongera sana Henry 14, huyo rafikiyo ana mapenzi ya dhati. Huo ni ugonjwa wa mapenzi.
 
Gonorhea hiyo wahi Hospital Utakuwa mgumba ukichelewa Ooooh. Na sasa hivi limekuwa gumu sana kutibika.
 
Gonorhea hiyo, wahi tiba haraka sana
 
Na Mimi kila nikikojoa zinatoka noti za elfu tano nifanyeje zitoke noti za elfu kumi au dollali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…