What is UTI ???.Huu ni ugojwa ambao Watanzania asili mia 95 (95%) hawaujui vizuri.Hata baadhi ya matabibu wamekuwa wanachanganya wagonjwa kwa kiwango kikubwa katika kutoa elimu ya afya kuhusu UTI.LAKINI pia alieongoza kwa kwa kiwango kikubwa kuwapotosha Watanzania kuhusu UTI ni nini, ni daktari bandia Dr.Mwaka aliefungiwa kutoa huduma ya tiba mbadala.Huyu kamwaga sana Sumu ya uongo kwa sababu alikuwa anafundisha kupitia redioni na kwenye tv.Kwa faida ya wale wataopata nafasi ya kusoma mada hii basi watakuwa wameilewa UTI ni nini.UTI ni maambizo yeyote kwenye njia ya mkojo.Na maambikizi kwenye njia ya mkojo kwa kiwango kikubwa husababishwa na magonjwa ya ZINAA.Magonjwa ya zinaa ni kama;Kisonono(neisserie gonorrhroe),Clamydia trachomatis,Trichomonas,fungus(candidiasis),herpes simplex virus type 2.Dalili kuu za magonjwa haya ni maumivu wakati wa kukojoa,kuwashwa wakati wa kukojwa,mkojo kuwa wa njano,wakati mwingine kukojoa damu au usaha.UTI kwa kiwango kidogo inaweza kuletwa na magonjwa ambayo sio ya ZINAA kama kichocho cha kibofu cha mkojo(Schistosoma haematobium),vimelea vya Escherichia coli(E.coli),vimelea vya Staphylococcoci na Streptococcoci)Kwa hiyo msaada kwa huyu mwenzetu ni kwamba inaonesha dhahiri ana maambukizo kwenye njia ya mkojo(UTI)Na hayo maambukizo yaweza kuwa kwa kiwango kikubwa ni magonjwa ya zinaa ambayo kwayo hata wewe ni mhanga.Kama wewe hujisikii kitu na tayari mmefanya tendo la ndoa basi wewe utakuwa 'carrier'unaeeneza kwa wengine bila ya wewe kuumwa.Au mwenzako atakuwa amechepuka.Namna sahihi ya kugundua tatizo la UTI ni kupima mkojo,utoko wa njia ya mkojo kama usaha kwa kufanya wet preparation,gram stain na culture.Matibu ya UTI yanategemea na aina ya vimelea vitakavyogundulika kwenye vipimo.Ref.kuhusu UTI unaweza kusoma kwa undani kitabu cha Merck Manual of Medical information.