Ndugu Matindi94,
Kujibu maswali yako napenda kukupa uzoefu kama ifuatavyo kwa sababu mimi pia ni mdau katika kilimo cha Macadamia.
Macadamia (au karanga mti kwa kiswahili) ni zao jamii ya nuts au karanga kama vile korosho.
Hustawi vizuri katika maeneo ambayo hulimwa parachichi, kahawa au migomba pia wataalamu ktk tafiti wanasema mahali popote ambapo mti ya matunda damu (tomato tree) hustawi basi macadamia hustawi.
Hali ya hewa nzuri kustawi macadamia ni nyuzi 15 celcius hadi 25c joto kali huathiri ukuaji na kutengeneza maua. Pia ni afadhali ya baridi kuliko joto kali hivyo mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, na maeneo ya Mbinga, Lushoto nk inaweza kustawisha.
Ili kupata mavuno mazuri wanasisitiza kupanda miche ambayo ipo grafted, kinyume na hapo utapata miti ambayo haizai vizuri na kuchelewa kuzaa kwani iliyofanyiwa grafting huanza kuzaa mwaka wa tatu na ile ambayo haijafanyiwa grafting huanza kuzaa mwaka wa sita au kumi.
Tafiti zinaonesha spacing nzuri kupanda ni 8m x4m yaani mstari kwa mstari mita 8 na mti hadi mti mita 4 na hekta moja yaani ekari 2.471 ni miche 312
Hekta moja inatakiwa kutoa mavuno ya tani 3 hadi 5 au zaidi kama unatunza vizuri.
Ila kwa data zilizopo Kenya mti mmoja huzaa kuanzia kilo 20 hadi 80 kwa mwaka kutokana na aina ya mti na utunzaji.
Kwa wastani bei ya kilo moja ni Tsh 4,500 ha Tsh 6,000 ambazo hazijabanguliwa (Nut in Shell or NIS)
Pia kuna siku nilitembelea Shoppers Plaza kuna Supermarket niliona 150g za roasted macadamia zinauzwa Tsh 65,000 (je, 1,000g au 1kg itakuwa shilingi ngapi?)
Katika nuts zote macadamia ni the best kwa ladha na bei sokoni.
Mimi nilipanda mwaka jana hekta moja yaani ekari 2.471 miche 312 pia kwa Tz kupata miche grafted ni mtihani kwani hata jamaa wa SUA nilienda ili miche yao siyo grafted labda kama mwaka huu wamefanya.
Mimi miche nilipata kampuni ya Lima wapo Vwawa Songwe na bei ya mche mmoja grafted ni Tsh 7,500
Kwa uzoefu wangu kupanda macadamia ni rahic kuliko parachichi kwani inavumilia ukame kuliko parachichi.
Kwa data zilizopo hakuna zao lenye kipato kikubwa kwa ekari moja ukiacha Vanilla.
Mfano Afrika kusini, baada ya kutoa gharama zote mkulima hupata rand 374,400 yaani Tsh 64,584,00 kwa hekta moja (ekari 2.471) kwa macadamia ambazo hazijabanguliwa.
Na huko Australia ambapo ni native wa hili zao wao mkulima mmoja ana wastani wa hekta 5 yaani ekari 12 hupata wastani wa dola 150,000 (Tsh 349,500,000) kwa mwaka.
Njombe tumeanza kupanda ila si kwa kiasi kikubwa tatizo ni namna ya kupata miche bora iliyofanyiwa grafting pia miche ni gharama sana.
Uzuri wa hili zao nuts zake huweza kuhifadhiwa na kutunza kwa muda wowote na soko ni kubwa kuliko uzalishaji dunia nzima.
Kwa Afrika mashariki Kenya inaongoza kwa uzalishaji na kwa sasa Afrika kusini inaongoza Afrika na duniani ikifuatiwa na Australia.
Binafsi napambana angalau niwe na ekari mia moja ambazo tayari nimeshazipata na kilichobaki ni upandaji naamini kwa miaka hii mitano ya awamu ya tano nitakuwa nimemaliza kupanda ekari zote mia.