Msaada: Baba yangu ana tatizo la kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno

mlete kwa YESU anaokoa kama una imani njoo pm nikuunganishe kwa mtumishi wa Mungu naamini ataokolewa
 
Pole sana ameanza hilo tatizo lini..?alishawahi kupata ajali..?akafanye ct scan na mri atakua na space occupying lesions ila ku rule out mpk afanye scan
Ni miaka 3,hakuwahi kupata ajali yoyote.umri ni 70
 
poleni sana. mpeleke hospitali na kwenye maombi pia, hii dunia ina mambo mengi. Mungu akuongoze na kukupeni nguvu
 
Pole sana, ndugu yangu hapo bila shaka mzee wako atakuwa na convulsions /seizures /Epileps/kifafa
Hiyo inatokana na shida kwenye ubongo ambayo inapelekea ubongo kutoa kiasi kikubwa cha nerve impulse (umeme) bila mpangilio.
Sababu inaweza kuwa ni ugongwa ambao alikuwa nayo tokea utoto lakini ukatulia baada ya kutumia dawa au sababu nyingine ila sasa umerudi tena.
Sababu nyingine inaweza kuwa kitu tunaita SOL(space occupying lesion) kwenye ubongo.
Kitu cha msingi hapo ni kwenda hospitali na kufanya CT scan na EEG, na Nerve conducting studies, ba vipimo vingine kama FBP hapo watajua tatizo haswa linalomsumbua mzee wetu.
 
Nashukuru sana na wewe kumbe umeona hiyo hosp. Yaani ni hovyo sana hawajui kutumia vipimo halafu bei mbaya sana. Hivi huwa hakuna uchunguzi wa ubora wa huduma zap?
 
mlete kwa YESU anaokoa kama una imani njoo pm nikuunganishe kwa mtumishi wa Mungu naamini ataokolewa
Acheni utapeli wenu kabisa.uliona wapi maombi ni dawa. Mpeleke hosp akapate tiba sahihi.maombi ni wizi na kumzidishia maumivu mgonjwa
 
Pole sana Ndg, Kama walivyokwisha kuasa wachangiaji waliotangulia mpeleke hospitali mapema, kama una bima ya afya ya NHIF Itakuwa vizuri ktk kupunguza gharama za vipimo. Kama upo mikoa ya Kusini huko nafikiri Mbeya referal sidhani kama wanafanya vipimo vya CT Scan na EEG (unaweza kuulizia) lakini Dodoma hospitali ya Benjamin Mkapa wanafanya CT Scan na Kipimo cha EEG kinafanyika Mirembe hospitali, otherwise Unaweza kumpeleka Muhimbili. Hizi hospitali nilizokutajia ni za Umma japokuwa zipo hospitali (Dar, Mwanza) binafsi zinatoa huduma hizo ila kwa gharama za juu kidogo japokuwa watalaamu ni walewale.
 
Kuna jamaa yangu mama yake mdogo alikuwa na tatizo kama hilo kalazwa Muhimbili muda pamoja matibabu mengi bado hukupona haraka.
Jamaa zake wakamshauri ampeleke kwenye maombi sasa hivi majuzi namuulizia vipi mgonjwa hali yake ikoje kwa ssa? akanijibu "usicheze na Yesu" baadaye ndo akanipa mkanda mzima kuwa aliombewa akatapika sana mpaka sasa nimzima kabisa!!
Nilitaka kujua ilivyokuwa kwasababu hali ya mgonjwa nilikuwa naifahamu sema tu jamaa alikuwa na haraka ya safari. Baadaye ndo nikampigia simu akanipa mkanda habari ndefu kuhusu maombi.
Alinitajia jina la Mchungaji aliyemuombea kwamba anaitwa PARAPANDA na kwamba yuko Dar es salaam Tanzania . Japokuwa jina lake linatisha ila kwa vile muhusika anadhibitisha mama yake alipona haina shida.Nakushauri nenda Hospitali lakini pia
Mtafte huyu mchungaji
 
Unampa Habari za Yesu, ila unataka aje sirini! we ni mpuuzi sana, unataka umtapeli?
Mbona habari za Yesu wengine wanazitangaza kwa vipaaza sauti ili kila mtu asikie?
[emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Kifafa mkuu hiyo ilimtokeaga dadaake na rafiki yangu na alipona kwa tiba za jadi japo amefariki kwa ugonjwa mwingine kabisa,alikuwa anang'ata na kutafuna hadi mchanga
cc. Mzizi mkavu mshana jr

Hivi kifafa huwa kinaweza kuanzia ukubwani?
 
Mwanangu alipima mri na ct scan muhimbili, marumba psychiatric hosp na bugando med centre kote ziro nikapambana na hali yangu dogo yupo poa sana
 
Tatizo kaanzia ndani ya hiyo miaka 3,Asante kwa ushauri mkuu
 
Aisee kwa sasa nipo Sogwe,na magonjwa kwa sasa yupo Moshi,ni ngumu kimtafuta pasipo chanzo.asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…