Msaada! baba yangu anakohoa mfululizo

nsalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
1,189
Reaction score
1,240
Wanajamii naombeni msaada. Baba yangu anakohoa mfululizo kikohozi kikavu, ameshaeenda hospitali akapewa mucolin ametumia amemaliza lakini bado tu. Akarudi tena hospitali akapewa dawa nyingine ya kikohozi pamoja na dwa ya minyoo lakini hakuna nafuu yoyote. Baba yangu pia ana tatizo la kisukari je lina uhusiano wowote na kikohozi hicho? Nisaidieni jamani baba yangu apate kupona.
 
Akapime kwanza magonjwa yote.afu uje tena hapa kuleta feedback.
 
Akapime kwanza magonjwa yote.afu uje tena hapa kuleta feedback.

asanteni sana kwa ushauri mlionipa. Nitafanya hivyo then nitakuja na majibu hapahapa
 
Mucolin ni dawa ya watoto,wengi huuzia watu dawa ili wapate hela tu,nenda kwenye pharmacy yoyote,ulizia dawa inaitwa Menthodex,itamsaidia,japo bei yake iko juu kidogo.kuna nyingine ina box la njano,imechorwa simba,nayo ni nzuri,nimelisahau jina lake.
 
Mnunulie dawa inayotwa mkojo wa punda, nasikia ni dawa nzuri kwa kikohozi.
 
Mucolin ni dawa ya watoto,wengi huuzia watu dawa ili wapate hela tu,nenda kwenye pharmacy yoyote,ulizia dawa inaitwa Menthodex,itamsaidia,japo bei yake iko juu kidogo.kuna nyingine ina box la njano,imechorwa simba,nayo ni nzuri,nimelisahau jina lake.

Menthodex sio dawa mkuu, ile ni Kama cofta! Hiyo ya box la njano uliyosema inaitwa cadiphen. Ni nzuri sana.
 
Menthodex sio dawa mkuu, ile ni Kama cofta! Hiyo ya box la njano uliyosema inaitwa cadiphen. Ni nzuri sana.
exactly,Cadiphen....kuna menthodex za maji,sio vile vipipi,mimi huwa inanitibu vizuri mno.
 
Kaka Fadhili ni kweli baba yangu ana kisukari karibu miaka kumi na mbili sasa ana tatizo la kisukari. Samahani nimechelewa kujibu.

Mpe pole sana, MIAKA 12 anaumwa tu. Inaniuma sana. Fanya yafuatayo:
1. Soma maelezo katika link ifuatayo ujifunze kwanza kisukari ni nini, na kwanini kisukari hakitibiki hospitalini, Bonyeza: Kisukari/Diabetes | maajabuyamaji.net

2. Utakwenda pia kujifunza namna ya kutumia maji kujitibu na kila ugonjwa ikiwemo kisukari katika link hii, bonyeza: Jitibu kwa kutumia maji | maajabuyamaji.net

Ningependa pia kujuwa upo mkoa gani tz
 
Asante sana kaka Fadhili kwa mchango wako. Mimi nipo Dar es Salaam, Iila baba yangu yupo Moshi maeneo ya Msasani CCBRT.
 
Asante sana kaka Fadhili kwa mchango wako. Mimi nipo Dar es Salaam, Iila baba yangu yupo Moshi maeneo ya Msasani CCBRT.

Nitumie namba yako katika 0769142586 napita maeneo hayo kila siku hata kesho nitapita pia, nikiwa maeneo hayo nitakupigia tuonane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…