Msaada: Biahara isiyohitaji msaidizi na bila kuharibu ratiba yangu

mpatto

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Posts
766
Reaction score
1,031
Habari wanabodi,

Mimi ni mfanyakazi sekta binafsi, nimejikusanya na sasa nina kama 1M hivi.

Nataka kuifanyia biashara lakini sijui nifanye biashara ipi, maana ama nitafute mtu wa kunifanyia hiyo kazi au niache kazi na kuofanya biashara.

Yote kati ya hayo ni magumu kwangu kwa maana kwa biashara inapokuwa changa ni vigumu sana kukua kwa haraka kama hauifanyi wewe direct. Mfano, kuuza duka n.k
Pia kuacha kazi na kuanza kufanya biashara ni risk sana provided biashara haikufanikiwa. Ni kweli ninafahamu kuwa ukitaka kuwa entrepreneur ni lazima uwe risk taker, lakini tukumbuke kuwa hizo risks lazima ziwe calculated kwanza.

Sasa, nimekuja hapa kwa nyie wadau ambao ni great thinkers na of coarse some of you have such experiences, muweze kunishauri, kwamba kwa mtaji huo wa 1M naweza kufanya biashara gani real isiyohitaji msaidizi au kuharibu ratiba zangu zingine!

Natanguliza shukrani

Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta bodaboda used ya mil. 1 mpe kijana azungushe. After all kama biashara ikiwa ngumu, una asset tayari so unaweza i dispose na ku recover capital yako.

Wazo tuuuuu!!!????
 
Jenga guest house classic lakini ya vyumba vichache kama vyumba 8 tuu.. kila siku unauhakika wa kujaza.. Fanya ujenge kila mkoa.
Ile unastaafu, kazi yako kuzungukia assets zako..


Updated: kumbe mtaji wa milion moja.. fungua tuu banda la chips..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…