Msaada; Biashara ya kusafirisha abiria

Msaada; Biashara ya kusafirisha abiria

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Habari wakuu,
Nina wazo la kufanya biashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia basi ndogo aina ya Costa ambayo nategema kufanyia mkoani lakini bado nafanya utafiti nijue ni route ipi nzuri hasa itakayokuwa na Barabara ya lami

Naomba kujua mambo yafuatayo kutoka kwa wazoefu wa hii biashara

1. Bei ya Costa hasa(Nissan Civilian)ni kiasi gani kwa kununua hapa nchi au kuagiza na inakuwa imetembea km ngapi?

2. Costa hii ina uwezo wa kubeba wastani wa watu wangapi(level seat)? Na vipi kuhusu uimara wake?

3. Gharama za kulipia bima na usajili kwa ajili ya kutumia kwa biashara ni kiasi gani

4. Kwa route ya kwenda km 100 naweza kuingiza kiasi gani kama itaenda Mara 2 kwa siku ukitoa gharama za mafuta nk

5. Pia kwa hapa Dar Costa ya namna hio inalaza sh.ngapi kwa siku?

6. Chochote ninachohitaji kujua kuhusu biashara hii ikiwemo changamoto zake kwani sijawahi kabisa kuifanya

N:B
Safari ya km 100+makadirio ya nauli ni sh. 5000

Karibuni kwa msaada wa mawazo

280px-Civilian4-1.jpeg
 
CC@kitabakilo,bilengeh niliona mahali mlichangia kwa uzoefu mkubwa naombeni mawazo yenu.
 
Changamoto hizi ukiziweza utafaidika -ale dereva. -ale kondakta. ale trafi. ale teja. Ile serekali. Ile gari naona kwako itafika sound!
Na ndio maana naomba msaada wa wadau, hivyo hata wewe nisaidie maswali ya hapo juu.
 
Hata ukifuga Kuku kideri kitakula ukibisha kideri kisile atakula muuza madawa utalipa hio price lazima pia kila biashara lazima u pay price no mater how hata shetani huwa anataka agano la damu "we talk with one's who pay for the price"
 
Ungeomba ushauri KABLA hujanunua hiyo gari, Mimi ningekushauri uachane na hiyo biashara na uwekeze kwenye kilimo!
Kila mtu hua anawazo lake tuna vitu vingi vyakufanya pia tunamawazo mengi Sana kama mtu ametoa wazo lake na ameonelea hapo panafaa usimpe wazo jingine ila mjengee misingi imara yakusimama katika wazo lake nakulifanya kua tija sahihi ila kumuongezea wazo nikumuongezea muda wakutafakakari nakua katikati afanye lipi aache lipi hili niupotevu wa muda it's fine mjengee hoja katika kile anachokiamini ili afanikiwe na afungue mawazo yake tena kwenye jambo jingine
 
Utafanikiwa ukinunua direct kutoka JAPANI. Usisubutu kununua kwa mtu ambayo imefanya kazi Tanzania [emoji1241].
Unachosema ni kweli ndio maana nimeuliza Bei ya kuagiza au kama sivyo basi showroom
 
Kila mtu hua anawazo lake tuna vitu vingi vyakufanya pia tunamawazo mengi Sana kama mtu ametoa wazo lake na ameonelea hapo panafaa usimpe wazo jingine ila mjengee misingi imara yakusimama katika wazo lake nakulifanya kua tija sahihi ila kumuongezea wazo nikumuongezea muda wakutafakakari nakua katikati afanye lipi aache lipi hili niupotevu wa muda it's fine mjengee hoja katika kile anachokiamini ili afanikiwe na afungue mawazo yake tena kwenye jambo jingine
Sawa!
 
Back
Top Bottom