mkuu natumai umeona fursa na umeamua kutafuta taarifa muhimu kabla ya kuingia kwenye ununuzi/uanzishaji wa biashara hiyo, nikupongeze kwa kuona vyema fursa na kutafuta taarifa za awali
Nikuweke sawa tuu katika aina za gari kuna Toyota coaster pia kuna Nissani civilia hizo ni gari mbili tofauti kabisa japo zote zinatoak japanio, toyota ni miongoni mwa brand za ukweli sana hasa hiyo coaster ukiilinganisha na nissan civilian, coaster inauwezo wa kuishi miaka mingi sana na ndo maana unaweza kuona namber b ama c ipo barabarani kama daladala tena mji mgumu kama Dar, nasema mgumu maana magari hayawezi kuishi miaka mingi kutokana na kazi kubwa yanafanya pia na ubovu wa barabara zetu
Nirudi katika bei za magari hayo Coaster ipo juu katika bei na hizo coaster pia zinatofautian maana kuna box na mayai ila 55-95 ila nimejaribu kuangalia ya mwaka 2008 inazidi 95 iko katika hali nzuri kabisa ila nazungumzia coaster mayai, ila mkuu kwaupande wa civilian mpaka inakufikia mkononi kwa ambayo imetumika zaidi ya miaka kumi unaweza ipata hata kwa 45, 50 mpaka 60 na inakuwa nzuri kabisa
Kwanini wengi wanapenda civilian? civiliani ni bei nafuu ukilinganisha na magari kama mistubish, isuzu, na kina toyota na ndomaana wengi wanazinunua kwa wingi na hesabu yao kubwa inakuwa ni miaka miwili hela yao inakuwa imerudi yote kama mambo yakienda kama yalivyopangwa nikiwa namaanisha Mungu kaondolea mbali ajali na majanga mengine, pia hesabu yake inafikika hasa ile ya 100 000 mpka 120 000 (120 000 rejea juu) kwa watu wanaofanya biashara hapa Dar kwahiyo mtua najua ikifika miaka miwili chombo bado kitakuwa na hali nzuri na akiamua kukiuza si chini ya 20M kinaondoka haraka , kwahiyo anakuwa na faida yakutosha na akiamua kuendelea nacho ni juu yake.
Hesabu kwa Dar mkuu ni kama nilivyoonyesha ila kwa nje ya mji sifahamu sana , ila unaweza fuatilia na ukapata majibu mazuri, ila mkuu biashara ya magari inafaida nzuri sana tena sana mie nikushauri ka umetia nia wee fanya upembuzi uanzishe maana kikupasacho wewe ni usimamizi wa ukaribu, pia ni kuomba Mungu maana biashara zote zenye hela hazikosi changamoto nyingi ila kubwa ni hiyo ya usimamizi an kujua namna ya kupambana na madereva na makondakta maana bila kupata dereva anaejielewa utaona mambo ni magumu kupita kawaida na unaweza jutia kujiingiza kwenye biashara.
MKUU karibu katika biashara ya porini biashara ya tractor si mbaya kama utakuwa na usimamizi ama ukiwa na muda wakuwa nawe pori
Kila la heri