Msaada: Biashara ya mchele.

0909Hekima

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2013
Posts
226
Reaction score
65
A.alykum wana JF, nina mtaji wangu pia ninaona fursa kubwa juu ya hizi biashara za nafaka, nimeamua ku segment na kuchukua biashara ya mchele, masoko nayaona ila upatikanaji wake ndio imekuwa challenge kwangu na nimeona niliwakilishe ili ndugu zangu mpate nipatia mawazo ili nami pamoja nanyi tunufaike! Ahsante.
 
Kama masoko unayaona nini cha zaidi unatafuta?
 
Am also interested in this mkuu,let them flow
 
Kikubwa nachotafuta ni upatikanaji wake ambao nitauchukua na kuufikisha katika sehemu niliyodgamiria ufike. Asante. Sunshow
 
Nenda ifakara mchele kibao nenda mwenyewe kule kule uazisome bei...achana na walanguzi wa mjini
 
Nenda ifakara mchele kibao nenda mwenyewe kule kule uazisome bei...achana na walanguzi wa mjini

taarifa sahihi, kwenye biashara ya nafaka ni muhimu sana. Kufika kwenye chanzo kutakusaidia. Biashara unapata faida wakati wa kununua.
 
Mkuu, SOKO la mchele umeliona halafu haujui sehem ya kupata mchele??..Uko mwingi sana mkuu, nenda shamba! Usitume mtu, kama una pesa yako mkononi NENDA SHAMBA, Ifakara, Kyela, Kahama...Haujasema tu uko wapi!!
 
Nipo dsm kaka mkuu. Shukran sana
 
nitafute kwa namba hizi 0654 100 960, 0768 165 289, kama kweli upo serious
 
sema unahitaji kiasi gani? isije ukawa unahitaji kwa ajili ya retail ..... mchele ni mwingi mno; changamoto kwenye biashara ya nafaka huwa ni usafirishaji, enzi za train mambo yalikuwa powa lakini siku hizi kwa magari wenye mitaji mikubwa wakisikia sehem fulani kuna uhitaji wa chakula fulani wanawahi haraka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…