Msaada.. Biashara ya samaki

Msaada.. Biashara ya samaki

Ubungo Mataa

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2018
Posts
411
Reaction score
725
Nimepewa wazo la biashara ya Samaki wabichi. Unachukua samaki wabichi aina kadhaa kutoka kwa wavuvi Bagamoyo kwa vipimo vya ndoo unaepeleka moja kwa moja kwenye maduka ya samaki Kariakoo. Jamaa anasema inalipa vizuri ila hana uzoefu.

Naomba mwenye uzoefu au anaefanya biashara hii anipe A B C, kama una ndugu au rafiki yako anafanya hii naomba uniunganishe nae.

Comment au DM ipo wazi.

Asanteni!
 
Mbona Bagamoyo unawatoa mbali Sana?? Sijui Faida itakuwaje, Ila Jitahidi utoe pale ferry! Otherwise utaumia..

Biashara ya samaki haieleweki!
 
Owky.. Asante kwa ushauri mkuu.

Sijajua bado lakin swala la bei kwa Ferry na Bagamoyo huwa zinapishana kiasi gani. Ila jamaa alisema tuu Bagamoyo.
 
Nenda ktk hayo maduka ya samaki Kariakoo uulize wananunuaje then nenda kwa wachuuzi bagamoyo uulize wanauzaje pia hapo hapo utakutana na wazoefu watakuongeazea maarifa namna gn wanazisafilisha na taarifa zingne muhimu
 
Back
Top Bottom