Msaada: Biashara yangu inapata Mauzo hafifu

Msaada: Biashara yangu inapata Mauzo hafifu

Waheshimiwa nahitaji msaada kwenye hili, hivi inakuwaje mtu hauuzi kabisa dukani kwako kwa siku karibia 20 yani kila siku patupu tatizo linakua ni nini?

Binafsi nimefungua frame nauza mitumba ya kike(gauni) lakini niliuza siku 5 za kwanza tu ila sasa hivi mambo magumu mzigo ni kama umechacha sijafikia hata nusu ya gharama za mzigo.
location pia inachangia
 
Usisuburi wateja wa kuja dukani anza kupost mitandaoni

Piga picha nguo vizuri iwekee details post
Sponser ads utauza tu
Nimeanza kufanya hivo lakini response bado ni ndogoo nimejiunga huko facebook lakini bado
 
Inawezekana sana tu. Juzi nilienda kwa mtu mmoja yeye anafungua balo nyumbani kwake. Ana mdoli anavalisha kila nguo then anatupia picha wasap. Wateja wa jumla na reja reja mpaka anatuma nje ya mkoa aliopo.Alinihamasisha kwakweli.
inavutia sana katika mandishi
 
Chochote utakachoamua ni sawa ila hakikisha unaondoka na funzo fulani la marketing.

Well, tengeneza mtandao wa wateja, jiwekee mikakati ya jina la aina ya bidhaa unazouza.

Nilifanya hatua hizi kuwa na mtandao wa wateja hasa kwenye WhatsApp contacts list / Facebook na Insta.

1.
Nilikuwa nalipia facebook ads inatangaza, insta na facebook, naweka settings accordning to aina za wateja/watu naotaka kuwafikia.

2.
Nahakikisha kuna namba za simu, na picha nzuri za bidhaa,ilikuwa mtu akipenda aki click inampeleka kwenye namba zangu za simu akitext namba inakuwa kwenye phonebook yangu

( provided contact synchronised kwenye clouds ili siku ukipoteza simu unazi recover).

3.
Nilikuwa na mpango kazi wa 3 months naruka week mbili mbili kupandisha ads.

4.
Network ikakua na hata sometime unauza lakini unaweza act kama middle man kipindi huna mzigo, mtaji ni contacts list uliyo nayo.

Fanya haya hata ukihama ulipo unaweza hama na baadhi ya wateja wako hii ina kuwa unapiga miguu yote, ila kuhusu kuhama liangalie kwa umakini hata huko uendako pia, kupiga one two za maombi/dua, ndumba ziwepo kama extras [emoji28].

Tyrone KG
Nashukuru sana
 
Ebu nikusaidie tiba ya muda mfupi, kwanza unatakiwa uwe mtu wa maombi sana uwe mchaji kulingana na Imani yako.

Kisha, chukua MDALASINI kama ni kijiko kimoja changanya na KARAFUU kijiko kimoja, tia kwenye sufuria yenye maji chemsha kwa DAKIKA 11 tu, epua kamwage eneo lako la biashara.

Ikiwa mwanzoni uliuza vizuri ikafuatia mfululizo kwa kutouza bas kuna tatizo kiroho.

Ukifanya nilichokuelekeza kama ni usiku wa leo kesho utawaona wateja.
 
Usisuburi wateja wa kuja dukani anza kupost mitandaoni

Piga picha nguo vizuri iwekee details post
Sponser ads utauza tu
Yes siku hizi biashara zinahitaji matangazo ya mtandaoni,ukiuza kwa staili ya kizamani ya kukaa kwenye kiti unangoja wateja hupati kitu.
Maana kuna wafanyabiashara wa kutoka mbali wanakuja mtaani kwako wanafanya delivery kwa wateja nyumba hadi nyumba na wewe wanakupita tu.
Lakini sababu nyingine pia biashara ikiwa mpya usitegemee mauzo kwa haraka,huwa inachukua muda sana hadi ije kuwa stable.
 
Ebu nikusaidie tiba ya muda mfupi, kwanza unatakiwa uwe mtu wa maombi sana uwe mchaji kulingana na Imani yako.

Kisha, chukua MDALASINI kama ni kijiko kimoja changanya na KARAFUU kijiko kimoja, tia kwenye sufuria yenye maji chemsha kwa DAKIKA 11 tu, epua kamwage eneo lako la biashara.

Ikiwa mwanzoni uliuza vizuri ikafuatia mfululizo kwa kutouza bas kuna tatizo kiroho.

Ukifanya nilichokuelekeza kama ni usiku wa leo kesho

Yes kabisaa
Tafadhali naomba upite kwenye page yangu unisupport Allana's Closet (@allanah_closet) • Instagram photos and videos
 
Back
Top Bottom