Msaada:Chaguo sahihi kielimu

Farmer82

Senior Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
183
Reaction score
39
Wadau hodi kwenye jukwaa..baada ya kutembelea jamiiforum kama guest kwa miaka miwili mfululizo,hatimae jana 15/09/2013 niliamua kujiunga rasmi na mtandao huu,ambao umejaa vichwa vyenye mawazo mapana sana...kwa kuanzia tu ndugu zangu,nahitaji msaada wenu wa kimazo kwa mimi kijana mwenzenu! Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 35,baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 2000 sikuweza kuendelea na masomo ya chuo kikuu kutoka na kukosa principal za kuweza kunivusha,baada ya hapo,niliamua kuingia kujitafutia kipato kwa njia tofauti na niliweza fika mpaka nchi za wenzetu,lakini sikuona mafanikio yoyote mwisho wa siku niliamua kurudi nyumbani!hapa nyumbani niliporudi niliingia moja kwa moja kwenye kilimo ambapo awali nilipata misukosuko sana mpaka kukata tamaha lakini hatimae sasa nimeanza kuona matunda ya kilimo!na mbali ya kulima,pia nimenunua magunia kadhaa na kuyaifadh tayari kwa kuyauza hapo miezi ya mbeleni!Nisiwachoshe sana wadau,msaada wa mawazo ninao uomba toka kwenu ni juu ya kozi sahihi mimi kujiendeleza kielimu,kozi nilizokua napendelea ni za arts hasa Law,Bus Admin na Procurement,je ndugu zangu kwa uzoefu wenu,kozi hizo kutokana na umri wangu na miaka niliyokaa benchi bila kusoma na shughuli ninazofanya kwa sasa ni kozi gani ambayo ingenifaa zaidi!najaribu kuangalia na kwa future incase mambo ya biashara yakienda kombo na kama ikatokea fursa ya ajira basi nami niwe ni mshindani mmoja wapo na si kua umri wangu uwe kikwazo,nahisi kuna baadhi ya field hata umri ukiwa umekwenda kidogo wanaweza kukuajiri au hata ukianzisha kitu chako kutokana na taaluma yako. Lakini lengo langu kubwa ni kua niendelee na biashara zangu huku nikiwa na taaluma yangu ya kitu fulani pembeni.. Asanteni wadau nasubiri ushauri wenu kwa unyenyekevu
 
Karibu Kaka. Wakati ukisubiri Wataalamu wakushushie vitu, pata machache mepesi kutoka kwangu:
1. Elimu Haina Mwisho. Hata ungekuwa na Umri wa Miaka 65, ruksa kuingia Shule kusoma
2. Elimu ni Ufunguo wa Maisha. Elimu itakuwezesha kuyaona mambo kwa upana wake
3. Mwajiri mzuri na ajira nzuri ni wewe mwenyewe na Mradi/Biashara yako uliojiajiri. Usione watu wamevaa nadhifu wakiendea kwenye ajira za kuajiriwa, ni watumwa wa mishahara ya mwisho wa mwezi, wengine ni wadokozi, wala rushwa, wabadhirifu wa Mali ya Mwajiri, madeni mpaka shingoni, n.k. Huenda uko vizuri kuliko wengi wao! Ukijipanga vizuri ukafanikiwa, wewe ndio utakuja kuwaajiri Wahasibu, Wanasheria, Maofisa Ugavi, n.k.
4. Katika Kozi ulizotaja hapo juu, ninaipigia upatu Business Admin., pamoja na sifa nyingine, ni "Kozi Malaya". Soma ujiajiri ili uajiri na sio uajiriwe!

Wakongwe wanakuja kukudadavulia ma-vituz!
 

Asante sana ndugu yangu,kwa kweli umenipa courage kubwa sana hasa hapo katika kipengele cha tatu na cha nne!nashukuru sana ndugu yangu
 
kwanini usianze na Kozi ya Ujasiriamali, nadhani unaweza anza soma hata kwa level ya diploma, then ukaanza hiyo Business admin Baadae

Kwa kufanya hivyo utaimarisha kilimo/biashara zako na utakuwa unafanya kwa ustadi zaidi....hiyo BA unaweza soma hata kwa Masafa....namaanisha Open and distance learning ukifanya hivyo biahsra zako hazitaathirika hata kidogo

all the best
 

Asante sana ndugu yangu,huu kwa kweli ni ushauri mzuri sana,hata mimi wazo langu ni kufanya open kwa level ya degree!ila mkuu mimi sivifahamu vyuo vinavyotoa kozi ya ujasiriamali kwa level ya diploma,je unaweza kunisaidia mkuu,either kiwe Morogoro au Dar es salaam!asante sana
 

Ujasiriamali....nakushauri kama utaweza UDBS- Chuo kikuu cha dar es salaam shule ya Biashara wana DIPLOMA ya Ujasiriamali pamoja na MA- ya ujasiriamali........cha msingi tembelea website yao ikiwezekana waandikie/wapigie/au watembelee kabisa.....Naamini itakusaidia kupanua mawazo yako na mwisho wa siku utafanya biahsara yakoi vizuri

Kila la kheri
 

Asante sana mkuu,kwa kweli umenipa mwanga wa kutosha!nitajaribu kuwauliza na Mzumbe kama watakua na kozi hii watakua wamenisaidia sana,maana shughuli zangu nyingi nafanyia Morogoro!Asante sana ndugu yangu
 
Kaka kwanza hongera sana kwa story yako,ukweli imenigusa na kunipa hamasa kubwa!ulifanya jambo la busara sana kuamua kurudi nyumbani toka ughaibuni na kuingia kulima moja kwa moja,maana kule ukipotea umepotea moja kwa moja,wapo vijana wengi wamepoteza dira ila wanahofia kurudi nyumbani wakati hapa ni nchi ya maziwa na asali,stress free iwapo utakua si mtu wa kung'ang'ania kazi za ofisi na ukaamua kupambana kwa fursa zilizopo kama kilimo...kuhusu suala la elimu mkuu,nadhani wadau wamekushauri vizuri sana!wewe cha kusoma ni kile ambacho unaona kitakuongezea knowlege katika ku manage na kupanua biashara yako,wazo la kusoma kozi ili uje kuajiriwa ilo hachana nalo kaka,unatakiwa kudream big na kuja kuwaajiri watu wa hizo kozi unazowaza kusoma ili uajiriwe!kwa hiyo hapo kozi nzuri ya kusnma ni business admin and entrepreneurship,kuhusu vyuo kama mdau aliyetangulia amegusia kua UDBS wanatoa kozi hiyo ila kwa Morogoro nahisi Mzumbe wana kozi hiyo pia...hongera sana mkuu,thats a move!wenzetu wana kamsemo kao kua "BUSINESS IS THE ONLY TO GET RICH" sijui ukweli wa usemi huo,lakini yote kwa yote nina amini umechagua a right path!all the best
 
Mkuu kwanza karibu sana, Naomba nitietie nyama kwenye swala la kozi ipi ya kusoma,nafkiri pale Mzumbe kuna kozi inaitwa BBA in Enterpreneurship hii itakufaa sana mkuu
 
Leo hata mimi nimefaidika, wakubwa mmetoa somo zuri sana, hata kwangu nimepata elimu zaidi. namshukuru mleta mada na wachamgiaji pia.
 
Leo hata mimi nimefaidika, wakubwa mmetoa somo zuri sana, hata kwangu nimepata elimu zaidi. namshukuru mleta mada na wachamgiaji pia.

Mkuu wanasema ukitupa mada yako jamiiforum wengi wataondoka na kitu kipya kichwani..
 
Mkuu kwanza karibu sana, Naomba nitietie nyama kwenye swala la kozi ipi ya kusoma,nafkiri pale Mzumbe kuna kozi inaitwa BBA in Enterpreneurship hii itakufaa sana mkuu

Asante sana kwa kunijulisha ndugu yangu,nadhani nikipata pale Mzumbe itakua nafuu sana kwangu,maana shughuli zangu zote ni Morogoro!
 
Leo hata mimi nimefaidika, wakubwa mmetoa somo zuri sana, hata kwangu nimepata elimu zaidi. namshukuru mleta mada na wachamgiaji pia.

Tuko pamoja mkuu,ndio maana mimi naipenda sana jamiiforum hasa jukwaa ili la UJASIRIAMALI
 
Mkuu wanasema ukitupa mada yako jamiiforum wengi wataondoka na kitu kipya kichwani..

Ni kweli kabisa mkuu..na nimeipenda kauli yako hapo juu kua "Business is the only way to get rich"
 
Kwa wale waliosoma mpaka degree moja au mbili na kisha kuanza kazi kwa maana ya kuajiriwa, wengi pamoja na uwezo wao wa kujimudu kimaisha hawafurahii sana kuwa waajiriwa.....

wengi wanatafuta namna kila leo za kuwa wafanya biashara, wajasiriamali au waajiri...lakini uoga mwingi na uzoefu kidogo pamoja na muda hafifu huwafanya kufeli kabla hata ya kuanza.....

Kwako...kwakuwa umeshaanza katika upande huo wa maisha (i.e kujiajiri) nakushauri soma kozi za biashara kwa minajili ya kupanua ufahamu na kuongeza ufanisi katika biashara zako, usifikirie kabisa kuajiriwa kwani pia kuna vikwazo chungu tele ambao wahitimu wa vyuo wanakutana navyo kupata ajira, na hata wakizipata bado sio suluhisho la hali duni ya maisha.....
kwa hivyo soma kozi ya biashara lakini ukiwa na mentality ya kupanuka kimawazo na kiundeshaji ili uwe mfanyabiashara wa level za kina mzee 'More' huko mbeleni...
 

Asante sana mkuu kwa ushauri mzuri,kwa kweli nimezingatia ushauri wenu,na moja kwa moja nazama kwenye kozi kusoma kozi za biashara,ili niwe na wigo mpana katika kufanya mambo kwa ufanisi..asante sana mkuu
 
oh asante sana hata mimi ngoja nijipange niongeze ujuzi japo diploma tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…