Wadau hodi kwenye jukwaa..baada ya kutembelea jamiiforum kama guest kwa miaka miwili mfululizo,hatimae jana 15/09/2013 niliamua kujiunga rasmi na mtandao huu,ambao umejaa vichwa vyenye mawazo mapana sana...kwa kuanzia tu ndugu zangu,nahitaji msaada wenu wa kimazo kwa mimi kijana mwenzenu! Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 35,baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 2000 sikuweza kuendelea na masomo ya chuo kikuu kutoka na kukosa principal za kuweza kunivusha,baada ya hapo,niliamua kuingia kujitafutia kipato kwa njia tofauti na niliweza fika mpaka nchi za wenzetu,lakini sikuona mafanikio yoyote mwisho wa siku niliamua kurudi nyumbani!hapa nyumbani niliporudi niliingia moja kwa moja kwenye kilimo ambapo awali nilipata misukosuko sana mpaka kukata tamaha lakini hatimae sasa nimeanza kuona matunda ya kilimo!na mbali ya kulima,pia nimenunua magunia kadhaa na kuyaifadh tayari kwa kuyauza hapo miezi ya mbeleni!Nisiwachoshe sana wadau,msaada wa mawazo ninao uomba toka kwenu ni juu ya kozi sahihi mimi kujiendeleza kielimu,kozi nilizokua napendelea ni za arts hasa Law,Bus Admin na Procurement,je ndugu zangu kwa uzoefu wenu,kozi hizo kutokana na umri wangu na miaka niliyokaa benchi bila kusoma na shughuli ninazofanya kwa sasa ni kozi gani ambayo ingenifaa zaidi!najaribu kuangalia na kwa future incase mambo ya biashara yakienda kombo na kama ikatokea fursa ya ajira basi nami niwe ni mshindani mmoja wapo na si kua umri wangu uwe kikwazo,nahisi kuna baadhi ya field hata umri ukiwa umekwenda kidogo wanaweza kukuajiri au hata ukianzisha kitu chako kutokana na taaluma yako. Lakini lengo langu kubwa ni kua niendelee na biashara zangu huku nikiwa na taaluma yangu ya kitu fulani pembeni.. Asanteni wadau nasubiri ushauri wenu kwa unyenyekevu