Nipo na computer yangu inatumia window 10. Tatizo kuu ni hili swala la bundle consumption. Inanyonya sana kiasi kwamba ndani ya dakika 3 nikiiacha moderm On nakuta nimetumia mbs zaidi ya 30..Kwa makadirio ya haraka ni zaidi ya mbs 10 kwa dakika.
Nimejaribu kucheki kwenye setting pamoja na kuzima metered connection lakini bado tatizo linaendelea..sina utaalamu sana wa mambo haya ndio maana nimekuja kwenu wakuu muweze kunipa mwongozo..
Currently najikuta natumia almost 1 GB kwa siku bila kudownload kitu chochote wala kucheki videos. Msaada tafadhali.
1. Stop background apps, na pengine kuna updates huwa zinafanyika ndani kwa ndani
2. Check if hujaseti autodownload
3. Probably hacked?
4. Some people wanafungua program nyingiii kwa wakati mmoja.
5. Your search engines can be the source of trouble
Fohadi Unatakiwa uweke off metered connection mbili.Wewe umeweka tu moja.Sasa hivi nenda settings>update and security>Advanced options>download updates over metered connections>kisha weka off
Fohadi pia unatakiwa ujitoe kwenye windows insider program.Nenda kwenye internet browser yako kisha type kwenye google engine "signin in window insider program" kisha ikishafunguka sign in kisha utaona option ya kujitoa katika window insider program ambayo ndiyo huwa inaupdate window kila saa na kula bando.
Hizo ni windows update. Hujawahi update laptop yako ndio maana. Solution ya haraka kufanya hyo connection kuwa metered. Uki connect modem fungua ile icon ya wifi/Ethernet pale chini then bonyeza connection ya modem yako na uchague Properties. Itakapo kupeleka washa Metered Connection. Hapo basi haitwa download update zozote tena mpka uchague mwenyewe
Ilikuwa huru. Weka GB 10 iache PC ifanye inachotaka, baadae utakuwa huru kabisa. Nilikuwa na hilo tatizo nikaamua kufanya hivyo, sasa naweza acha moderm on hata saa zima bila hofu. Update kwangu nimeziweka kuwa automatic.