Msaada: Connection South Sudan

Msaada: Connection South Sudan

magee

Senior Member
Joined
Jun 3, 2009
Posts
130
Reaction score
21
Habari wanajamvi.

Mi ni mzalishaji wa bidhaa za chakula hasa sembe, mchele brown na white (mbeya kyela), maharage nk. Ningependa nipanue wigo wangu, natamani kufanya biashara na kenya na sudani kusini,ila zaidi sudan kusini tatizo connection na namna ya kupata taarifa sahihi za kodi na malipo mengine na logistic kwa ujumla.

Naombeni msaada wenu wakuu.

Nawasilisha.
 
mazao ya chakula selikali inazuia kutoa nje .
kuna kampuni kubwa za kilimo kama Kapunga na jingine lipo mngeta kilombero wana product tangu za mwaka jana hawaja uza.
Nilisha wahi ongea nao wanalia na serikali
 
Asante kaka.....nitazidi tafuta taarifa,nilitembelea wzrani wakasema mchele hauko kwenye zuio.nitarudi tena kwao.
 
Hapo ndo utashangaa watawala wetu! Unapoanza kulima hakuna chochote wanachokuchangia lkn Kwenye kuuza wanakuzuia duh,,! Inasemekana s,sudani kuna Biashara nzuri sana Tatizo USALAMA,,!
 
Mi huwa nafanya biashara ya viungo vya chakula Juba na Kampala.....kule biashara ni nzuri sana ....ila kwa sasa hakuna usalama ...manake nimepeleka mzigo wa viungo kama tani 40 mpaka sasa njia kuingia interior zimefungwa,hakuna usalama, yapata mwezi mzima sasa...
 
Mkuu bado wafanya hii biashara?
 
Mhh unataka kujilipua huko Nchi haina serikali utawezaje kufanya biashara huko...
 
Back
Top Bottom