Rhesus ni aina ya antigen ambazo hupatikana kwenye chembe chembe nyekundu (red blood cells) za watu wenye Rh+ blood group. Hivyo watu hawa hawana Antibody kwenye damu yao dhidi ya Rh positive antigen.
Watu wenye Rh -ve blood group hawana hizi antigen, hivyo wakiwekewa damu kutoka yenye Rh +ve wnatengeneza Antibody ambazo hushambulia chemechembe nyekundu zenye Rh+. Vivyo hivyo kwa mama mwenye Rh -ve blood group akizaa na mwanamume mwenye Rh + blood group, na ikatokea mtoto akawa na Blood group ambayo ni Rh +ve, basi damu ya mtoto ikichanganyika na ya mama itasababisha mama atengeneze antibody dhidi ya chembe chembe nyekundu zenye Rh +ve antigen. Kwa bahati nzuri damu ya mama na ya mtoto haichanganyiki wakati wa ujauzito, ila wakati wa kujifungua damu ya mtoto inaweza kukutana na damu ya mama, hivyo mama anaweza kutengeneza antibody dhidi ya chembe nyekundu zenye RH +ve za mtoto, antibody hizi hazina madhara kwa mtoto huyu kwa kuwa zimetengenezwa wakati akizaliwa.
Hizi antibody hubaki mwilini kwa mama, na zina uwezo wa kupenya na kwenda kwa mtoto, hivyo mtoto wa pili naye akiwa ni Rh +ve, anibody hizi hupenya katika placenta na kwenda kushambulia chembe nyekundu za damu (red blood cells) za mtoto aliye tumboni, hivyo kusababisha upungufu wa damu kwa mtoto aliye tumboni na hata kusababisha kuharibika kwa mimba.
Natumai nimetoa maelezo ya kuelezea Rhesus incompatibility na mdahara yake kwa mtoto ambaye hajazaliwa.