Msaada: Dar to Iringa na Boxer naombeni uzoefu wenu

Sikushauri hasa kipindi cha masika na mvua nyingi kama hiki, nakushauri jaribu kiangazi... Boxer inaweza kuteleza hasa kama mvua itakua imenyesha na pia chain haitaki maji Kwa umbali mrefu, utajikuta chain imekatika njiani afu usiku.. hakuna rangi utakayoiacha kuiona...
 
Nunua zile feni za kichina iweke mbele ya engine pale maana sijui hali itakuaje😂
 
Manina mpaka rangi ya gold asee

Kikubwa jamaa fuata ushauri wa Huyu mtu [emoji115]
 
Kuna mwingine alisafiri na pikipiki toka Dar hadi bukoba kwa wazazi wake lengo alike nayo na kurudi nayo.

Alipofika nayo bukoba baba yake akamuuliza kwa hiyo unesafiri na hii pikpiki toka dar hadi hapa bukoba akasema ndiyo.Akampa mkono kumpongeza akasema hongera sana wewe jasiri uko vizuri.Akatoka akaenda kuchukua gongo la mti akaanza kumpiga nalo kwa nguvu akamwambia mbwa wewe kwa nini uhatarishe msisha yako na lipikipiki mwendo wote huo ukipita mipori nk unataka kutuletea msiba hapa.Hiyo hela ya mafuta si ungepanda ndege.Akamtandika na akachoma na pikipiki yenyewe moto

Toka siku hiyo hadi leo hawaongei na baba yake.
 
Mi naona ungefanya utafiti wa watengeneza boksa

Ujue boksa inatembea umbali upi bila kupumzika then tafuta kilometer za dar to iringa
 
Sawa ila it is not a very good idea.kuna risk nyingi zilizojificha.
 
Na tangu hapo ningechoma nyumba yake na undugu ungekua umekufa kihivyo.
 
Mi naona ungefanya utafiti wa watengeneza boksa

Ujue boksa inatembea umbali upi bila kupumzika then tafuta kilometer za dar to iringa
Boxer mbeya dar masaa kumi kasoro
 
Safari yako inawezekana kwa asilimia 98 ukiachana na vitisho.

Amka asubuhi winda basi za kwenda mbeya au iringa kisha fatana nayo hapo mikumi au gari za mafuta ilio njema fatana nayo.

Boxer ipo vizuri ila kikubwa hakikisha unaipa serves ya kutosha na cha kuzingatia ni oili badirisha kila unapo taka kufanya safari ndefu.

Hata ukitaka kufika mbeya unafika fresh
 
Ulitumia masaa mangapi kwenda Dodoma-Dar
 
Hahahaa......nimecheka sana.

Wazee wengine wakorofi sana
 
Eti ulitaka kutuletea Msiba....
 
Nafikiria kununua BMW GS 1200 kufanya adventure bongo
 
Ok mm naswali kidogo hapa jamii forum

Kuna watu wanasafiri UMBALI mrefu mfano dar Mwanza kwa pikipiki 150cc?

JE wanatumia siku ngapi kwa huo UMBALI wa km 1100


Mafuta Lita ngapi?

Changamoto za barabarani?

Asante familia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…