Msaada: Dawa ya Degedege

nakwede97

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2021
Posts
946
Reaction score
2,478
Wapendwa nakuja kwenu mnisaidie dawa ya degedege Kwa mwanangu anateseka jamani kila akipata homa hiyo hali inamkuta.

Nisaidieni nimehangaika mie jamani, ana miaka mitatu tu.
 
Tafuta kinyesi Cha tembo, mugeshee na kumywesha Kila unapomuogesha.
Pia Kuna majani pori kwakihehe huitwa lwenyi ni kiboko ya degedege( picha ya hayo majani ni kesho)
Nitashikuru ukinionyesha picha
 
Degedege ni dalili ya ugonjwa fulani na heri utambue degedege si ugonjwa!

Kitaalamu degedege hujulikana kama CONVULSION

Hio inaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali kama vile Malaria mbaya, Meningitis ( uvimbe katika tabaka la nje la ubongo), kifafa na nk

Usitafute dawa muwahishe hospitali apewe matibabu!!!

Sent from my iris50 using JamiiForums mobile app
 
Degedege hospitalini! Sawa lakini siafiki
 
Hujakosea Kila akipata hata homa ya mafua makal inamkuta ni akiumwa tuuu ndo hua inamjia Tena akiwa na homa tu
 
Mavi ya ngombe yamekataaa kufanya kazi kwake

Ng'ombe umepata wapi hilo neno maana alieshauri kasema Tembo.

Fuata ushauri wa kitaalam na hayo mambo mengine yafuate pia ukiamua.
 
Chief upo sahii , maana ata homa ikiwa kari kwa watoto inasababisha iyo degedege
 
Pole kwa kuuguza huu ugonjwa mbaya sana mwanangu alitibiwa hospitali zote kubwa Muhimbili,Tumbi,Milembe,Malumba Psychiatric hosp,Bugando zote ziligonga mwamba tanhu akiwa na miezi 6 kaja pona akiwa na miaka 8 kwa dawa za kienyeji nilihangaika sana hadi umasikini ulinikamata. Pambana ukikosa majibu nifanye kufuatilia aliyemtibu ni mzee 1 wa Iringa namba sinazo tena ila nikifuatilia naweza unganisha dot. Pole sana kwa kuuguza huo ugonjwa siyo mzuri kabisa ndg.
 
Usisite kutupa namba ya huyo mzee au mrejesho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…