Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
Ocimum basilicum kisayansiKwa jina jingine huitwa KIVUMBASI
Wapendwa nakuja kwenu mnisaidie dawa ya degedege Kwa mwanangu anateseka jamani kila akipata homa hiyo hali inamkuta.
Nisaidieni nimehangaika mie jamani, ana miaka mitatu tu.
Ungepiga picha watu wauone ulivyo itawasaidia wengi mpendwa.Mimi wangu nilimpeleka hospitali, nesi aliyekuwepo ni mama mtu mzima akanielekeza mahali nikanunue dawa ya kienyeji niondoke na mtoto haumwi!!
Kuna mti unaitwa mchipukizi, ukiuona ni mkavu kabisa kama umekufa. Ukikata kipande na kukiloweka masaa kama 8 kinachanua vibaya sana. Unamuogeshea hayo maji na toka hapo hakupata tena!!
Ungepiga picha watu wauone ulivyo itawasaidia wengi mpendwa.
Kwenye Lwenyi na mavi ya tembo hapo umeongea vema kabisa.. Pale kijijini dawa ndo ilikua inatumika na watoto kupona haraka sana.Tafuta kinyesi Cha tembo, mugeshee na kumywesha Kila unapomuogesha.
Pia Kuna majani pori kwakihehe huitwa lwenyi ni kiboko ya degedege( picha ya hayo majani ni kesho)
Holly grass...yana harufu kaliHaya ndio hayo majani ambayo hupondwa pondwa na kuogeshea au kumpukutia mtoto.View attachment 2675965View attachment 2675967
Nini yanaweza kuwa madhara yake asipotibiwa na kupona?Pole kwa kuuguza huu ugonjwa mbaya sana mwanangu alitibiwa hospitali zote kubwa Muhimbili,Tumbi,Milembe,Malumba Psychiatric hosp,Bugando zote ziligonga mwamba tanhu akiwa na miezi 6 kaja pona akiwa na miaka 8 kwa dawa za kienyeji nilihangaika sana hadi umasikini ulinikamata. Pambana ukikosa majibu nifanye kufuatilia aliyemtibu ni mzee 1 wa Iringa namba sinazo tena ila nikifuatilia naweza unganisha dot. Pole sana kwa kuuguza huo ugonjwa siyo mzuri kabisa ndg.
KifafaNini yanaweza kuwa madhara yake asipotibiwa na kupona?
Mavi ya tembo atapata wapi mjini au maduka ya asiliTafuta kinyesi Cha tembo, mugeshee na kumywesha Kila unapomuogesha.
Pia Kuna majani pori kwakihehe huitwa lwenyi ni kiboko ya degedege( picha ya hayo majani ni kesho)
Sio Kila ugonjwa utibika hospitaliniNaomba kufahamu sababu ya kutokuafiki hospitalini
Hamna dawa ya degedege hospital nimehangaika na wangu miaka 7 hola hospital zote nzito nchi hiiDegedege ni dalili ya ugonjwa fulani na heri utambue degedege si ugonjwa!
Kitaalamu degedege hujulikana kama CONVULSION
Hio inaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali kama vile Malaria mbaya, Meningitis ( uvimbe katika tabaka la nje la ubongo), kifafa na nk
Usitafute dawa muwahishe hospitali apewe matibabu!!!
Sent from my iris50 using JamiiForums mobile app
Pole mkuu mie 8 yrsHamna dawa ya degedege hospital nimehangaika na wangu miaka 7 hola hospital zote nzito nchi hii