Msaada dawa ya kuvuta wateja

Msaada dawa ya kuvuta wateja

Wakuu mwenye kujua dawa ya kuvuta wateja naomba connection maana kuna business yangu nimefanya kila niwezalo ili kuvuta wateja nimetoka kapa.

Biashara kama haina wateja basi kifuatacho ni kifo cha biashara ili tusifike huko ni vizuri kujaribu namna nyingine ambazo zinaweza kuleta tija.

Nahitaji dawa ya kuvuta wateja.
Mkojo wa punda nusu lita changanya, utiti utitiri kilo moja na asali ibrand pamoja kisha paka mlangoni na dirisha ukinuia kwa lugha yoyote kuwa wateja wajae mpaka ukose cha kuwauzia.

Ila kabla hapo hakikisha biashara yako kuna bidhaa zote pendwa kulingana na takwa la wateja na eneo husika, pili toa huduma kwa kumsikiliza na kumwelewa mteja katika kutaka kumtosheleza uhitaji wake bali pia kuonyesha kujali thamani ya fedha alokuletea tatu jenga mazoea ya kupita na kuona namna wahudumu wanavyohudumia wateja nne ukaribu na ujirani na waliokuzunguka.

Kwa leo niishie hapa ikishindikana ntarudi kupa dawa moja kiboko
 
Hiyo kiboko ni ipi mkuu?

Mchawi mkubwa wa biashara ni location mkuu na uchangamfu Kwa wateja , angalia hapo ulipo Kuna muingiliano mkubwa wa watu , kama hakuna aisee hama maramoja tafuta sehemu sahihi
 
Dah ndumba hadi kwa wateja ndio maana kwenye manunuzi tunapata vizunguzungu wengine hatuelewi daaaaah hatari sanaaaa
Unapita kwenye biashara ya mtu kwa lengo la kununua viatu unajikuta umenunua na begi na mazaga mengine. ..kumbe jamaa wanatuwekea ndumba sisi wateja tununue tu bila breki.

Nyie waamini ndumba mtakuwa kuni siku ya mwisho
 
Zipo mkuu kama upo kusini nikupe connection
Wanasema kizuri kula nandugu MAisha yenyewe yasasa yamejawa na husda hivyo lazima utembee nayo hivyohivyo
 
Unafanya biashara gani kwanza??

Isijekua unauza biblia karibu na msikiti au quran nje ya kanisa.
 
Tizama location

Tizama nguvu ya competitors wako

Tafuta nguvu ya Mungu,acha uhuni dogo

Nguvu za Mungu zitakusaidia sana kufanya mambo yako.
 
Nenda kwa pusha mwambie akupe stiki moja.

Nyonga washa vuta.

Mawazo yatakujia kichwani tu nini ufanye ili biashara yako isife.

Kama sio mtu wa stiki basi amka saa nane usiku ongea na MUNGU wako kwama maana muda huo akili imetulia pia.
hakika umeongea ukweli wala stiki wote wana mawazo mbadala
 
Back
Top Bottom