Msaada dokta wa mifupa

Msaada dokta wa mifupa

selestin john

Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
67
Reaction score
8
Wana JF,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 22 na mnamo 11/12/2012 nilipata ajari ya kuangukiwa na kitu kizito pajani karibu na goti na nilipopelekwa hospitali walinipatia dawa za kutumia tu na kuniambia niwe nakwenda kufanya mazoezi hospitalini hapo .

Lakini umepita muda mwingi sana hakuna unafuu kwa sababu mguu naweza kutembea kwa kuchechemea kidogo na siwezi kukunja mguu unajikunja kidogo tu na ni kama umekuwa mfupi hivi.

Naomba kama kuna mtu anamfahamu dokta bingwa wa mifupa anijuze niweze kuonana nae nitambue kama matibabu yanawezekana na gharama zake zinakuwaje?
 
Wadau nina ndugu yangu alivunjika mguu sasa hajapona.

Kama kuna mtu anamfahamu Specialist wa mifupa pls let me know.
 
Wadau nina ndugu yangu alivunjika mguu sasa hajapona,kama kuna mtu anamfahamu specialist wa mifupa pls let me know

Kwanza pole kwa kuuguliwa na nduguyo,kuna mtaalam hapa anauwezo wa kumponya kwa miezi miwili.ukiwa tayari nitafute kupitia namba 0782568520.
 
Kwanza pole kwa kuuguliwa na nduguyo,kuna mtaalam hapa anauwezo wa kumponya kwa miezi miwili.ukiwa tayari nitafute kupitia namba 0782568520.

huu uhuni. mtaliwa hela bure nq tatizo likawepo.
kawaida mifupa huwa inapona na kuunga yenyewe bila hata kupata matibabu.
muda tu huifanya iunge.

tatizo linakuja kama;
-kuna vidonda vyenye uambukizo
- haiko aligned vizuri na kuna nyama kati ya mifupa.

issue ni namna mfupa utakavyounga na muonekano wa sehemu iliyovunjika.

hapo ndipo madaktari wa mifupa wanafanya kazi zao.
kuna mvunjiko hata iweje hauji kuunga bila kudanyiwa operation na kuwekewa vyuma.

hawa wanajiita waganga wa kienyeji ni uhuni tu wanawafanyia wagonjwa na kuwalia hela.
mwisho wa siku wanarudi hospitali wakiwa wamechelewa na wengine hukatwa miguu kabisa.
 
Wadau nina ndugu yangu alivunjika mguu sasa hajapona.

Kama kuna mtu anamfahamu Specialist wa mifupa pls let me know.

anaishi wapi na hospitali gani ya karibu kwake?huduma za mifupa zinapatikana zaidi hospitali za kanda na mission.
 
huu uhuni. mtaliwa hela bure nq tatizo likawepo.
kawaida mifupa huwa inapona na kuunga yenyewe bila hata kupata matibabu.
muda tu huifanya iunge.

tatizo linakuja kama;
-kuna vidonda vyenye uambukizo
- haiko aligned vizuri na kuna nyama kati ya mifupa.

issue ni namna mfupa utakavyounga na muonekano wa sehemu iliyovunjika.

hapo ndipo madaktari wa mifupa wanafanya kazi zao.
kuna mvunjiko hata iweje hauji kuunga bila kudanyiwa operation na kuwekewa vyuma.

hawa wanajiita waganga wa kienyeji ni uhuni tu wanawafanyia wagonjwa na kuwalia hela.
mwisho wa siku wanarudi hospitali wakiwa wamechelewa na wengine hukatwa miguu kabisa.

hahahahaha, na wengine wanahitaji kufanyiwa ORIF.

sasa najiuliza huko kwa waganga wa kienyeji inakuwaje...
 
Back
Top Bottom