Msaada: Duka la nguo za watoto

Wadau mke wangu ameachishwa kazi juzijuzi. kwa vile kazi yenyewe haikuwa na mshahara mzuri ameniomba nimpatie mtaji afungue duka la nguo za watoto. Naombeni ushauri.. Je linalipa ?
Natanguliza shukrani zangu.
 
Ndo hobby yake mkuu, acha afanye kitu roho inapenda, ukimfungulia la utakavyo naye atafanya atakavyo
 
Wadau mke wangu ameachishwa kazi juzijuzi. kwa vile kazi yenyewe haikuwa na mshahara mzuri ameniomba nimpatie mtaji afungue duka la nguo za watoto. Naombeni ushauri.. Je linalipa ?
Natanguliza shukrani zangu.
Ndio inalipa sanaaa ila ubunifu kulingana na wakati msimu wa sikukuu ndio muda wa mavuno,ufunguz wa Shule as katika huo umri 5yrs ndio watakuwa wanaanza shule.Na kuandaa package ya watoto wachanga kwa mfano mtu akitaka kupeleka zawad ananunua as kila kitu kumhusu mtoto mchanga kitakuwepo depend na jinsia ya mtoto.To me its good idea.
 
Nimejifunza kitu hapa.
 

niliwahi kufanya karesearch nikatembelea maduka kadhaa kariakoo...

kuna wauzaji wa Diapers ambao wanaImport na kuna wa jumla ambao wanachukua kwa walioImport.

Kwa upande wa Nguo wapo wanaouza jumla wanaingiza mzigo wenyewe na kuna wanaolangua pale pale Kariakoo

anza na Nguo za Vichanga na za watoto wa kiume zaidi,unaweza kuweka upande wa vitoy vya watoto unaenda kusort kuna maduka ya wachina yana vitu vizuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…