Msaada Earth Rod ipi nzuri wakuu

Hizo zote ni chuma cha kawaida zimekuwa electroplated na copper Copper org 50k and above
 
Bado earth rod hiyo kwa 25 elfu hawezi kupata pure copper ambayo ndio standard.
 
We ndo fala kwelo
 
Mara nyingi ubora wa kitu unaangaliwa kwenye bei kwa mtu asiyejua/asiye na utaalamu juu ya kitu husika, hivi kweli ukute 8000 na 25000 halafu ushindwe kujiongeza tu hapo kwamba ipi Bora!

Back to the question ni kwamba hiyo Nene ndo nzuri/bora kwa uzoefu wa kwenye taasisi zetu. Nimeona zahanati na shule kwenye BOQ zao wote wanaagiza hiyo Nene, bati kama sio msauzi wa 51000 basi watachukua geji 28 ya 31000, saruji watachukua aina fulani kwa kuangalia namba zile nk nk

Kuna kawaida wanasema mchunga mbuzi akiwa porini na njaa ni kali Hana chakula basi ataangalia mifugo wake wanachokula hata kama hakijui na yeye ale hichohicho. Chakula hiko hakiwezi kuwa sumu kwake. Namaanisha serikali na makampuni ndo wamezoeleka kutumia vitu standard kwahiyo hata mlala hoi mwenzangu kama unapata tabu kuelewa vitu bora jaribu kuwaiga wao wanatumia kipi kisha kama uwezo unaruhusu basi jipapasepapase ujitutumue na wewe uwaige kwa matokeo bora katika shughuli yako
 
Kiufupi zote ni fake maana zinanasa na sumaku ...kupata eath rod og wa bei hizo hapo juuu ni uongoo
 
Sasa ipo hivi pure coper unaipata kwa 40000 yapo hayo machimbo k/koo unauziwa kwa bei ya jumla hao wanaouza 50000 na kuendelea ni wamenunua nao wanauza kwa faida na ili uijue hii ni pure basi chuma chake kinakuwa ile gold imekoza sana na kubwa kabisa chuma chake kina asili ya kupinda unaweza kukipindisha na mkono na ukakirudisha.
 
Siku hizi wafanyabiashara wanatupiga sana kwenye bei. Hata hizo fake wanaweka bei kubwa ili uone ni original. Kwa Tanzania bei sio criteria ya ku classify bidhaa kama ni original au fake.
Kama kuna criteria nyingine za kutambua bidhaa original au fake itakuwa bora kuliko kutumia bei.
 
Tupe hilo chimbo mtaalamu
 
Harafu kuna mtu ana-like comment kama hii. Kuuliza sio ujinga, kama unaona muelewa sana na huna shida ya kutoa msaada pita kando kimyaa, sio kudondosha uharo hapa..
Mimi binafsi nimefaidika na uzi huu kujua namna ya kujua ipi fake na ipi OG kwa kutumia sumaku, nipo katika ujenzi, hii imenisaidia.. Wengi tumenufaika, waliokhereka watakua wauza bidhaa fake.
 
Tatizo kuzunguka k'koo yote kulisaka hilo duka/maduka
 
Harafu ndo kiswahili cha hapo kwenu wewe na mama ako? Jifunze kwanza kuandika vizuri ngumbaru wewe
 
Eath rod original ni ile ya 45k nipe kaz hyo nije nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…