Naomba nikueleze hali halisi...
Kwa namna hilo gari lilivyogongwa inawezekana kutengenezeka ila halitakuwa kama mwanzo...wajanja watagundua kuwa limegongwa na kunyooshwa....
Ila ukweli ni kwemba litakugharimu si chini ya M 3 kulirudisha kwenye hali yake...
Ukiamua kuliuza hivyo lilivyo kama scrapper hutakosa M1.5 mpka M 1.8..
Ushauri wa bure....kama uchumi wako upo vizuri, uza hiyo kwa 1.5 M kisha ongezea kama 3.5M ili upate jumla ya 5 million..........
Nina uhakika ukiwa na milioni 5 ,utapata brevis nyingine kama hiyo namba C iliyotulia......bora usiwe na haraka wakati wa kutafuta.
Au kama si brevis na bado unapenda 6 cylinders, kuna GX 110 nazo zina bei ndooogo tu ukimvua mtu.
Ila kama uchumi haujakaa vizuri, peleka kwa fundi, umlipe kwa installment mpaka amalize kazi.......
Mwisho, trust me...hiyo gari haitapungua Milioni 3 kuinyoosha, rangi na matairi yaliyopasuka, taa, bushes n.k.
This is free advice...