Msaada: Faida na hasara za biashara ya mashine ya kusaga/kukoboa mahindi

Tuo Tuo

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
678
Reaction score
1,202
Habari za sasa,

Kwa wataalam wa hii biashara nataka niingie hii biashara.

Nipeni dondoo.
 
FAIDA ZAKE
1.Unawezq nunua umeme wa 20,000 ukapata faida 60,000 inategemea na bei na ubora wa kinu cha kusagia.

2.Pumba zq mqhindi ni dili sana Gunia ni 20k-30k.

3.Ukipata location nzuri unarudisha mtaji wako ndani ya miezi 8-12.

HASARA ZAKE
1.Ukiunguza mota hela itakayokutoka sio chini ya laki 5 kuisuka upya.

2.Ukiunguza mita unaweza kaa hata miezi bila kubadilishiwa so hapo unakua umekaa bila kazi.

3.Masika huwa ku a tabia ya umeme kukosa nguvu hivyo operator anaweza kuunguza mota aspokuwa makini.

4.Kuwa makini na utoaji huduma (Mfano kutoa unga wenye chenga)ukijichanganya kidogo tu wateja wanahama kurudi ni baada ya miezi.

5.Wafanyakazi kuiba mf.Anajinunulia umeme hata wa 5k ukiisha huo hela yote yake.

So far ni Biashara yangu pendwa ina faida sana Nakushauri uifanye I hope utanogewa.

Kqribu kwa maswali zaidi
 

Bado atataka kujua Anapataje mashine inayotoa ungamzuri au original
 

vipi tathmini ya mtaji
 
Mmemwelewa kweli..anataka mashne ya aina gani umeme au engine za disel! Biashara hi inachangamoto yake inategemea uko wapi UKO KIJIJINI AU MJINI.

ya umeme
 
Mtaji ukoje kwa anayeanza hasa Bei ya mashine ya kukoboa na ya kusaga
 
Minimum ni Million 7. Kama utanunua vitu used inaweza kuwa chini ya hapo, mfano mi wakat naanza vitu vingi vilikuwa used hadi bati za jengo. Nkatumia kama 4Millions tu

mashine ulinunua used nayo
 
Nashukuru sana kwa ushauri huu dahh!! Hii project nimepambana nayo Sana. Nipo hatua za mwisho kabisa, Mashine ianze kufanya kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…