Msaada: Gari gani linakula mafuta kidogo?

True binadamu Wana siri nyingi hasa hizi nchi zetu bila michezo ya kiblack market utoboi.
 
Hiyo Rav4 inayokushinda matumizi, ni cc ngapi?

-Kaveli-
 
chukua mpaka 1300
 
Nunua hybrid car mfano acqua au toyota prius.huta regret..hizi gari inaweza kwenda mpaka km 30 kwa lita moja.
 
Mkuu mimi hapa si shauri anunue yoyote kati ya hizi ulizo weka hapa...but ana option ya kutafuta hybrid car yoyote ya bei kama ya ist mfano Toyota Prius generation 2 ina range price yake 14-17m au toyota acqua...hapa issue ni mafuta, so kwa gari hizi za hybrid zipo fuel efficient na economy then ni reliable kuliko gari zote hapo juu.
 
Mkuu vipi Suzuki kei, Suzuki alto Daihatsu Terios Kid, na Toyota pixis hizi ni za cc zisizozidi 700 hivyo ni fuel efficient infact kwa suzuki kei inashare spares na virikuu so spea za kumwaga. Japo kibongobongo Suzuki kei ni gari ya zamani sana but hizi pixis na alto angalau.
 
Kwa kuwa unachohitaji ni kupunguza gharama basi nunua gari kati ya hizi suzuki kei hii spea zake nyingi, mafundi wengi, maana injini yake ni kama ya kirikuu. Tatizo la hili gari ni la kizamani na ukiagiza japani itakukost around 12M. Sikushauri ununue yard au la mkononi hivi vigari vya cc ndogo ni delicate sana so bora uagize tu angalau utapata chombo hakijatumika sana na utadum nacho miaka kadhaa. Ila ukinunua used ya bongo au yard jiandae simu yako kujaa majina ya mafundi na kwenda gereji kila wiki. Gari ingine nzuri ni Suzuki Alto hizi zipo bongo ila si nyingi so huenda spea zikawa na bei iliyochangamka. Gari nyingine ni Toyota Pixis hii vilevile bongo zitakuwa chache sana so spea zitakuwa zinasumbua. Daihatsu mira kuhusu spea hii sifahamu sana. Yote kwa yote kama lengo ni kupunguza gharama zako za usafiri na ili usave pesa zifanye kazi nyingine basi nunua Suzuki kei tena agiza Japan utakuwa umemaliza.
 
Gari hizi zenye cc sijui 600,( yaan cc below 1000) ni shida ni delicate sana, zina struggle ku keep up na issues za barabarani mfano speed, matokeo yake zinatembelea rpm za juu kidogo hivo fuel efficiency ya gari zenye cc ndogo na upo driving habit mbaya, trust me efficiency itakua ndogo kuliko gari yenye cc 1290…

So kama isssue ni costs za mafuta nunua hybrid car or else kama wataka gari ambayo ni non hybrid basi tafuta gari at least yenye cc 1000 mpaka cc 1300 na iwe na piston 4 na ukiweza pata yenye gear box ya CVT inakua safi zaidi.
 
Mkuu hizo hybrid sasa si inabid iwe imetembea KM ndogo sana maana nasikia ikiwa imetembea KM nyingi then ujue na betri lake ndo linaelekea mwisho hivyo si ajabu likanunuliwa leo then mwakani biashara imeisha au inawezekana kureplace je bongo yapo kweli?
 
Baadhi ya wabongo wanapenda kiongea sana utafikiria anachokiongelea anakimiliki.

Kuna watu walikuwa wanasifia TV ambazo ni Curved, nilinunua najuta, sasa hivi nataka kununua ambayo si curbed. Yaani ukikaa kwenye Angle uoni picha vizuri.
 
rafiki yangu, ni hivi, gari inakufa kama huzingatii service, sasa kwenye gari ya hybrid kinacho ua battery ya hybid huwa ni joto. na hili joto linakua linatoka na feni ya hybrid battery kuto zungusha upepo wa kutosha kupoza batery, but hili tatizo hutokea pale filter ya hybrid fen inapokua imeziba na uchafu.. na mara nyingi before issue haijafika wakati wa kuharibika gari inakupa worning light kwenye dasboard (inaitwa triangle warning sign) ambapo ukiwa na tendency ya kusafisha filter, basi bettery itadumu mpaka utachoka gari, na kuhusu repalcement ya hybrid battery, yes bongo zinakua replaced vizuri, mara nying ikifa battery itakua imekufa cell chache, sasa waweza opt kubadili cel iliyo kufa au ukiona vipi unabadili the entire battery pack.

kuhusu filter za hybid battery kwa gari kama toyota prius au toyota acqua, utakuta sit ya nyuma kwenye sehemu ya kuegemea kuna matundu yamewekwa kwa ajili ya ventilation, sasa wengi hawajui kama yale matundu ndo fen ya hybrid inapo vuta hewa kwenda kupoza battery lakini pia ndo sehemu filter ya kuchuja vumbi inakaa.

Kuhusu mdau alivosema hapo juu inatakiwa iwe imetembea km chache, ukipata yenye km chache ni well and good, but nyingi ukipata inakua ina km 100,000+ kwakua hizi gari zinatumika kama daily commuter kwa watu wanaokua wanazimlliki, na hizi gari unakuta mtu anaendesha kilometa nyingi on original battery packs.

Hybrid toyota prius is most reliable, durable car kuliko gari zote ndogo ambazo wadau wamezitaja hapo juu . but matunzo ni muhimu.
 
Baadhi ya wabongo wanapenda kiongea sana utafikiria anachokiongelea anakimiliki.

Kuna watu walikuwa wanasifia TV ambazo ni Curved, nilinunua najuta, sasa hivi nataka kununua ambayo si curbed. Yaani ukikaa kwenye Angle uoni picha vizuri.
mkuu ukitaka nunua hizi tv zenye vioo flats, you need to be very careful na display technologies,,yaan ununue kitu unajua unanunua nini unless utajutia mkuu. the same applies to unaponunua chombo cha moto, Tanzania wengi twanunua gari kutokana na trend, muonekano wa nje, pia plate numbers(kwa wale tunao nunua used bongo), people dont take time kujua technical and mechanical isues ambao ndo chanzo cha faults/ breakdown nyingi, matokeo yake lawama zinakua nyingi na unakua na namba za mafundi phonebook nzima.

pia nilicho andika ni ushauri tuu, but mara nyingi muomba ushauri anakua tayari ana chaguo lake kitambo, so akua anaomba ushauri kupata opinion zitakazo kazia uamuzi, no wonder why mtoa mada alikua specific kwenye gari alizo zi-list (( na nukuu : gari kama Pajero mini, Suzuki Jimny) hadi CC 1500 ni muafaka zaidi)
 
Ni kweli, nilikuwa na Flat ya Inchi 410 nikaipeleka kijijini nikanunua curved ya inchi 49 baada ya baadhi ya members wakisifia Curved TV kumbe hakuna kitu.

Naachana nayo nitachukua flat ya inchi 65 ili niangalie world cup kwa raha.
 
Ok thanks bei yake used ex japan nadhani haitakuwa below 15/16M
 
Baadhi ya wabongo wanapenda kiongea sana utafikiria anachokiongelea anakimiliki.

Kuna watu walikuwa wanasifia TV ambazo ni Curved, nilinunua najuta, sasa hivi nataka kununua ambayo si curbed. Yaani ukikaa kwenye Angle uoni picha vizuri.
Hii ya tv hata mimi imenikuta kwenye lg
 
Ok thanks bei yake used ex japan nadhani haitakuwa below 15/16M
Yes, kwa prius gen 2 price range yake ni hiyo, kimuonekano gen3 ndo nzuri ila inachangamoto ya kuunguza head gasket kwasababu ya overheating inayosababishwa na kufa kwa electric water pump...gen 2 kwakua ina mechanical water ambayo inazungushwa na belt so haifi kuzembe..

Kumbuka theme hapa ni kupunguza costs za matuta na sio appearance... appearance kama ni issue basi Prius gen 3 au prius V ndo inamuonekan poa but ni expensive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…