MSAADA:-Gari Gx100 lina miss kila wakati tatizo ni nini?

MSAADA:-Gari Gx100 lina miss kila wakati tatizo ni nini?

Rummashi

Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
43
Reaction score
6
Wakuu heshima kwenu, Jamani gari yangu salon ninabadili s plug kila wakati kwa ushauri wa mafundi lakini haichukui muda inaanza tena miss za ajabu, nimemwaga oil ila tatizo bado. kwa yeyote mwenye ujuzi tafadhali naomba msaada
 
shusha tank mwaga mafuta na kulisafisha kisha weka mapya

Pia kwa kuongezea hapo mkuu Rummashi, hakikisha unaweka petroli safi.
Angalia sana petroli yako unanunua wapi.
Kuna 'sheli' nyingine wanauza petroli chafu iliyochakachuliwa.
Sisitiza kuweka petroli safi wakati wote.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu heshima kwenu, Jamani gari yangu salon ninabadili s plug kila wakati kwa ushauri wa mafundi lakini haichukui muda inaanza tena miss za ajabu, nimemwaga oil ila tatizo bado. kwa yeyote mwenye ujuzi tafadhali naomba msaada
Tatizo hapo ni piston rings- unahitaji kubadilisha na kuweka mpya. kwa tatizo hili hata uweke plugs mpya, usafishe fuel tank, uweke fuel filter mpya- tatizo bado litabaki pale pale. Kwa uhakika zaidi perform diagnosis kwenye garage zenye hii huduma.
 
mkuu umenena maana nimesafisha tank mara mbili issue bado, na kunafundi mmoja alinishauri nikamuona sio ila nimeanza na first aid zote zimegoma, poa, ngoja january ipite maana... je unaweza kunipa approx .. za spare? na ni zipi maana mafundi wetu mkuu si unawajua tena? if u dont mind
 
mkuu aksante p'se hebu nipe maujanja ya pump ikianza kuchoka walau dalili zake ili nirelate na tatizo langu
 
Kuna plug inayofanya kazi ktk vipindi vyote vya hali ya hewa yaani baridi na joto, hivyo unatakiwa kujua ni plug ya mazingira gani, hot au cold. harafu na tatizo hilo pia linaweza kusababishwa na kuchoka kwa piston rings ambazo huzuia oil kufika kwenye chemba.
 
Pia kwa kuongezea hapo mkuu Rummashi, hakikisha unaweka petroli safi.
Angalia sana petroli yako unanunua wapi.
Kuna 'sheli' nyingine wanauza petroli chafu iliyochakachuliwa.
Sisitiza kuweka petroli safi wakati wote.

nini kimekufanaya uhisi kuwa misfire hii ni kwa sababu ya petrol chafu???hakuna sababu nyingine?
 
Tatizo hapo ni piston rings- unahitaji kubadilisha na kuweka mpya. kwa tatizo hili hata uweke plugs mpya, usafishe fuel tank, uweke fuel filter mpya- tatizo bado litabaki pale pale. Kwa uhakika zaidi perform diagnosis kwenye garage zenye hii huduma.

nini kimekufanya uhisi kuwa sababu ya misfire hii ni piston rings??hakuna sababu ingine?
 
Wakuu heshima kwenu, Jamani gari yangu salon ninabadili s plug kila wakati kwa ushauri wa mafundi lakini haichukui muda inaanza tena miss za ajabu, nimemwaga oil ila tatizo bado. kwa yeyote mwenye ujuzi tafadhali naomba msaada

kama umebadili plugs basi fanya yafuatayo
1.safisha nozzles
2.angalia fuel filter kama iko sawa

kama umesafisha nozzle na fuel filter iko sawa na gari bado ina miss kuna % nozzle zimekufa hivyo zibadilishe....ila ni muhimu kufanya diagnosis
 
Hapo chakufanya nenda kinondoni biafra kuna garage wana tumia computer watakagua gari yako kisha utaambiwa tatizo la gari yako. Mambo ya kubuniwa tatizo sio zuri bora uwe na uhakika. Mimi nilishakua na tatizo kama lako nikaenda kumbe ilikua ni oxygen sensor ilikua imekufa.
 
mkuu sio kila tatizo mashine inaweza kutambua kuna matatizo mengine ni madogo sana yanahitaji tu akili ya kifundi tuu mkuu??
harafu hizi mashine sasa hivi zimeleta mafundi waajabu ajabu sana na wavivu sana kiufundi kwa taarifa yako kama gari itakuwa haiwaki taa ya CHEK engine basi asilimia 90 haipimiki.

miss zipo za aina nyingi mkuu za mafuta? hewa na moto sasa hapa first aid ya uhakika ni kutambua kuwa hiyo ni miss ya mafuta au hewa au moto ukijua tu hivyo basi hakuna ugonjwa hapo.

mkuu kama utataka kupimiwa nitafute mimi nitakupimia bure ninamashine ya kupimia nichek 0717 228064 sana sana napatikana mwenge mkuu.
 
Back
Top Bottom