Msaada: Gari hii imeshindikana kuondoa miss

Msaada: Gari hii imeshindikana kuondoa miss

teac kapex

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
470
Reaction score
137
Ndg wapendwa naomba kusaidiwa juu ya tatizo nililokumbana nalo kwenye gari aina ya nissan vanete, gari hii ilikuwa nzima lkn kumetokea miss ambayo imeshindikana kutoka chanzo ni kwamba pale ilipoanza niligundua kuwa moja kati ya nozel haifanyi kazi hivyo nikaiondoa na gari ikawa vzr, baada ya siku tatu hali hiyo ikajirudia nikaona nozel nyingine sio nzr nikaitoa na gari ikawa vzr, bada ya siku chache hali ikajirudia tena nimebadilisha pampu, fuel filter, plug wire, spark plugs zote lkn tatizo liko palepale, sasa watalamu naomba msaada zaidi nimeleta mafundi 3 wote wanchofanya ni kubadili plug, waya, nozel na hakuna zaidi wanaondoka bila kuaga, natanguliza shukran.
 
7baef6196edad8ee3f76e76998caba7a.jpg
 
Kuna mtu mmoja kasema nijaribu kubadilisha control box hivi inaweza kuhusika?
 
Pole,gari ikishaanza kusumbua namna hiyo huwa wazo linalonijia haraka ni kuliuza kwa bei hata ya hasara,kwani inaweza kweli ikapona lakini inaweza isipone wakati imeshakulia hela kibao..
 
Nenda vijana garage karibu na SEMA muulizie awadh atakusaidia ni mtaalam wa gari injection
 
Kuna mtu mmoja kasema nijaribu kubadilisha control box hivi inaweza kuhusika?
Ni kweli kabisa mkuu kama control box imepiga shoti vitu vingi havitafanya kazi ikiwemo nozel, plugs, sensors na utafikiri ni vibovu kumbe ni vizima.

Hata mimi nilipata tatizo kama hili na nilipata hasara ya kubadilisha vitu vingi ikiwemo sensors, plugs, nozel n.k. kumbe ugonjwa ulikua control box.

Mtafute fundi mzuri wa wire apime hiyo control box.
 
Back
Top Bottom