FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Nina kagari kangu kanatatizo kwa muda sasa, ninapokua naendesha halafu wakati niko kwenye mwendo kuna wakati engine inakua kama inajipinguza speed (Rpm) na nikiachia accelarator pedal gari inakua nzito kama inajipiga stop engine hivi kwa muda then inaacha, na pia wakati nimesimama kwenye foleni, wakati wa kuondoka gari inakuwa nzito na sluggish, yaan inachelewa kuchanganya tofauti na ilivyokuwa awali. Nilishabadilisha Curburator (Throttle body complete), 'speed sensor' za kwenye gear box, na hata 'fuel filter' ya kwenye tank la mafuta nilisafisha pia. Sasa hii hali bado inaendelea na inanikera mno, nisaidieni kwa wenye utaalam na haya mambo.
Gari ni Toyota saloon car, automatic transmission.(Brevis)
Gari ni Toyota saloon car, automatic transmission.(Brevis)